Potyvirus helitessellati
Kirusi
Awali, mabaka ya kijani angavu na kijani iliyokolea huonekana juu ya majani (muundo wa mozaiki). Madoa madogo ya rangi ya njano iliyopauka hujiunda juu ya jani. Dalili huonekana kwanza katika majani machanga yaliyopo sehemu ya juu ya mmea. Dalili za hatua za mbele huonekana baada ya wiki 3+. Mimea hubaki ikiwa mifupi kuliko mimea ya alizeti yenye afya. Vichwa vya alizeti ni vidogo zaidi na huumbika vibaya. Mbegu huwa chache zaidi, na zinaweza kuwa na umbo dogo zaidi. Katika hali mbaya zaidi, majani hugeuka kuwa ya rangi ya kahawia na kisha hudondoka.
Hakuna matibabu ya kiasili ya kutibu ugonjwa huu wa kirusi. Tumia mbinu za udhibiti wa kiasili mbalimbali zinazojikita katika kuwadhibiti vidukari, sambamba na kudumisha mienendo bora ya kilimo ili kuzuia kirusi hichi kwa muda mrefu.
Hakuna kemikali yoyote inayoweza kutibu mimea iliyoambukizwa. Udhibiti hujikita zaidi katika kuzuia maambukizi kupitia udhibiti wa vidukari. Nyunyiza dawa za kuuwa wadudu punde vidukari wanapoonekana kwa mara ya kwanza, kabla kirusi hakijasambaa. Nyunyiza kwenye majani ya juu na kwenye majani ya chini pia ambapo vidukari hujificha. Usinyunyize dawa katika siku zenye upepo mkali ama kabla ya mvua kunyesha. Badili aina mbalimbali za dawa za kuuwa wadudu ili kuepusha mmea kugeuka sugu. Daima vaa mavazi ya kujilinda na fuata maelekezo yaliyopo kwenye lebo.
Kirusi Mozaiki cha Alizeti husababishwa na Potyvirus helitessellati na huathiri aina zote za alizeti ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na aina za alizeti mwitu. Mbegu zilizoambukizwa zinaweza kusambaza kirusi hicho kwa mimea mipya. Vidukari wa rangi ya kijani hubeba kirusi huyu kutoka kwenye mimea iliyoambukizwa hadi kwenye mimea yenye afya. Kirusi huyu husambaa upesi kipindi cha hali ya hewa ya joto, ambacho vidukari huwa wachangamfu zaidi. Kirusi huyu anaweza pia kusambazwa shambani kote na wafanyakazi ambao wanaweza kuwabeba virusi hawa mikononi mwao, kwenye mavazi yao, ama kupitia vifaa na zana za shamba zilizo na virusi hawa.

This page is powered by millions of live Plantix diagnoses. See where Kirusi Mozaiki cha Alizeti is spreading — district by district — with Crop Insights, part of Plantix Intelligence.