Alizeti

Baka la Alizeti

Alternaria helianthi

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Huathiri sehemu zote za mmea zilizo juu ya ardhi.
  • Madoa ya rangi ya kahawia iliyokolea, ya maumbo mbalimbali, huonekana.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Kupungua kwa upana wa shina na kipenyo cha kishada.
  • Upungufu mkubwa katika mavuno ya mbegu.

Inaweza pia kupatikana kwenye

0 Mazao

Alizeti

Dalili

Madoa ya rangi ya kahawia yanaweza kuonekana kwenye majani, shina za majani, shina za matawi, sepali, na kwenye petali za mmea. Kuvu huyu husababisha ugonjwa wa mabaka kwenye miche, na uozo wa kishada. Kwenye majani, vidonda hivi huwa vya rangi ya kahawia iliyokolea, vyenye ukingo uliopauka sambamba na mduara wa mwanga wa manjano. Kadri ugonjwa unavyoendelea, ukubwa wa vidonda huongezeka hadi kufikia takribani kipenyo cha sentimita 2-3 na baadaye huungana na kutengeneza kidonda chenye umbo lisilo la kawaida, na kisha kutengeneza baka na mnyauko wa majani. Eneo hizi huzungukwa na kanda ya klorotiki yenye sehemu ya kati iliyooza, ya rangi ya nyeupe ya kijivu. Madoa hujitokeza kwanza kwenye majani ya chini na kisha husambaa kwenye majani ya kati na ya juu. Kwenye mashina, vidonda huonekana kama madoa meusi ya mviringo, marefu ama yenye vifereji. Kwenye sepali na kwenye petali, madoa hufanana na yale yaliyopo kwenye majani, lakini hapa huwa na umbo dogo zaidi (kipenyo cha sentimita 0.5-2) na huchanganyika. Matokeo ya maambukizi haya ni kuibuka kwa mabaka na kupukutika kwa majani, kuharibika kwa maua na vishada vya mbegu, kunyauka kwa mimea, kubabuka kwa shina na hatimaye kufa kwa mmea. Pia, wakati mwingine, vishada vya maua huoza.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Ili kuuchochea udongo kujisafisha wenyewe baada ya mavuno yanayotangulia msimu wa vuli, inapendekezwa kwamba bidhaa za kiasili zenye Trichoderma spp. ama nyenzo za kibiolojia za kudhibiti pathojeni wa mimea (Bacillus spp., Pseudomonas spp.), zitumike.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia matumizi ya njia mseto zinazojumuisha mbinu za kinga sambamba na tiba za kiasili, ikiwa kama zinapatikana. Katika uoteshaji, tumia mbegu zilizotibiwa kwa dawa za kuuwa kuvu zenye imazalil na tebuconazole (dawa za kuuwa kuvu zinazofuata mfumo maalum). Katika kipindi cha kukua kwa mmea, kutumia dawa zenye cymoxanil (dawa ya kuuwa kuvu ifuatayo mfumo maalum), boscalid, na tebuconazole (dawa ya kuuwa kuvu ifuatayo mfumo maalum) kunaweza kudhibiti ugonjwa huu.

Ni nini kilisababisha?

Husababishwa na kuvu aitwaye Alternaria helianthi. Pathojeni huyu huishi kwenye mabaki ya mbegu na mimea. Mimea huwa hatarini kupatwa na maambukizi kuanzia kwenye hatua ya kuchipuka hadi kipindi cha mavuno. Ugonjwa huu husambaa kwa kasi katika hali ya hewa ya joto, kavu, yenye mvua zinazonyesha kwa kipindi fulani. Utumiaji kupita kiasi wa mbolea zenye naitrojeni huzidisha uharibifu wa mmea.


Hatua za Kuzuia

  • Fanya kilimo cha mzunguko kwa miaka 3-4.
  • Weka chokaa kwenye udongo wenye asidi.
  • Lima mashimo yenye kina kwa kutumia jembe lenye mkondo mmoja ili kuhakikisha mtiririsho mzuri wa maji kwenye udongo na kuondolewa kwa mabaki ya mimea.
  • Ulimaji wa udongo uliopo katikati ya safu za mazao huondoa gamba la juu la udongo na kuboresha mzunguko wa hewa kwenye udongo.
  • Hakikisha viwango sawia vya virutubishi kwa kutumia mbolea za fosforasi na potasiamu.
  • Kuotesha mazao mwishoni mwa msimu kunaweza kupunguza athari ya ugonjwa huu.
  • Tumia nyenzo mbalimbali zilizopo zinazozuia ugonjwa huu.

Pakua Plantix