Alizeti

Ubwiri Unga wa Alizeti

Golovinomyces cichoracearum

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa meupe ya unga unga kwenye majani na shina.
  • Majani yaliyoathirika yanaweza kugeuka kuwa ya njano na kisha kukauka.

Inaweza pia kupatikana kwenye

0 Mazao

Alizeti

Dalili

Mwanzoni, huonekana kama madoa meupe, ya unga, kwenye sehemu ya juu ya majani yanayoelea chini, yaliyozeeka zaidi. Baada ya muda, madoa haya hupanuka na kufunika eneo zima la jani. Madoa haya ya unga unga yanaweza pia kuonekana kwenye shina na kwenye sehemu za chini za majani, pindi madhara yanapokuwa makali zaidi. Majani yaliyoathirika hugeuka kuwa ya manjano, kisha huwa na rangi ya kahawia, na yanaweza kufa. Mimea iliyoathirika sana inaweza kudhoofika na kuzeeka mapema. Miundo midogo meusi ya mviringo inaweza kutokea ndani ya madoa haya meupe katika hatua za mbeleni za maambukizi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Nyenzo za kiasili kama vile spishi za Trichoderma na Bacillus subtilis, bidhaa zenye salfa, michanganyiko yenye potasiamu bikaboneti ama vioevu vya mafuta ya mwarobaini vinaweza kusaidia pindi vinapotumiwa mapema.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia kujumuisha njia mseto zinazotumia suluhisho za kinga sambamba na tiba za kiasili ama zilizo rafiki kwa mazingira. Dawa za kuuwa kuvu hufanya kazi vizuri zaidi pindi zinapotumiwa kama kinga ama pindi zinapotumiwa mwanzoni mwa dalili za ugonjwa. Hakikisha matawi yanafikika vizuri wakati unapoyapulizia dawa kwani pathojeni husambaa upesi katika mmea. Badili aina ya dawa za kuvu mara kwa mara ili kupunguza hatari ya mmea kuwa sugu kwa dawa fulani.

Ni nini kilisababisha?

Tofauti na magonjwa mengi ya kuvu, ugonjwa huu hustawi katika hali za joto, kavu, zenye kiasi kidogo cha unyevunyevu. Joto la mchana na ubaridi wa usiku huchochea kuenea kwa ugonjwa huu. Husambaa kwa urahisi kupitia hewa. Kuvu huyu haitaji uwepo wa maji kwenye jani ili kuliambukiza. Huendelea kuishi kipindi kisicho cha msimu katika mabaki ya mimea iliyoathirika na kwenye mimea mwitu inayoathiriwa kirahisi na pathojeni kama vile mualizeti mwitu. Matawi mengi yaliyosogeleana, yasiyopitisha hewa vizuri, huchochea hatari ya maambukizi.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zilizothibitishwa na za aina mbalimbali, zenye uwezo mkubwa zaidi wa kustahimili ama kuzuia ugonjwa huu.
  • Epuka kuotesha mimea mingi eneo moja ili kuboresha mzunguko wa hewa.
  • Badili zamu za mazao kwa kuotesha mimea yenye ustahimilivu mkubwa zaidi wa pathojeni.
  • Baada ya mavuno, ondoa na teketeza mabaki ya mimea iliyoathirika.
  • Epuka kutumia mbolea ya nitrojeni nyingi kupita kiasi.
  • Kagua mimea mara kwa mara, ukichunguza kwanza majani yanayoelea chini ili kugundua mapema uwepo wa madoa meupe.

Pakua Plantix