Alizeti

Mnyauko wa Alizeti usababishwao na Verticillium

Verticillium dahliae

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Majani hugeuka kuwa ya manjano, kuanzia sehemu ya chini kuelekea juu.
  • Hali hii ya manjano huathiri upande mmoja kwanza.
  • Shina linapokatwa, ndani huwa la rangi ya kahawia.
  • Mmea hudumaa na kufa kabla ya wakati.

Inaweza pia kupatikana kwenye

0 Mazao

Alizeti

Dalili

Rangi ya manjano huanza kuonekana kwenye majani yanayoelea chini. Mara nyingi, dalili huonekana upande mmoja wa mmea ama sehemu nusu ya jani. Mimea iliyoathirika hunyauka wakati wa mchana, hata pale inapomwagiliwa maji. Kadri mmea unavyoendelea kukua, madoa madogo ya rangi nyeusi yanaweza kutokea juu na ndani ya shina. Mimea iliyoathirika sana na ugonjwa huu hukua na kisha hufa mapema kuliko ile yenye afya, hivyo kupunguza ubora wa mbegu na mavuno.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa sasa hakuna njia ya udhibiti wa kibiolojia ama kiasili iwezayo kudhibiti kabisa ugonjwa huu. Kuongezea maada za kaboni kama vile mchanganyiko wa mimea kwenye udongo kunaweza kusaidia kuchochea viumbe hai vinavyoboresha rutuba na afya ya udongo na hivyo kumzuia pathojeni huyu. Matibabu kwa Nishati ya Jua: kufunika udongo wenye unyevunyevu na plastiki kipindi cha jua kali kunaweza kupunguza wingi wa kuvu kwenye tabaka la juu la udongo.

Udhibiti wa Kemikali

Udhibiti wa kemikali katika mnyauko wa alizeti usababishwao na Verticillium ni mdogo sana, kwani hakuna dawa inayopatikana kwa sasa inayoweza kuuwa kabisa kuvu pindi mmea unapokuwa umekwisha athirika. Dawa za kuuwa kuvu zinazowekwa kwenye mbegu kabla ya mbegu kuoteshwa zinaweza kusaidia. Weka dawa kipindi cha kuotesha, kwani vioevu vya majani haviathiri pathojeni wakaao kwenye udongo. Udhibiti wa kutumia kemikali daima unapaswa kutumika kama nyongeza ya njia nyingine za kinga, na kamwe si kama suluhisho la pekee.

Ni nini kilisababisha?

Husababishwa na kuvu wa kwenye udongo aitwaye Verticillium dahliae. Kuvu huyu huishi kwenye udongo, hata udongo ule usio na mmea. Huingia kwenye mmea kupitia mizizi na kisha kuzuia mtiririko wa maji. Husambaa kwenye udongo, zana za kilimo, mabaki ya mimea, na kwenye mbegu. Hali hizi huchochea ugonjwa huu: hali za joto la chini kwenye udongo (kati ya 15°C na 25°C), hali ya unyevunyevu mwingi kwenye udongo kipindi cha mwanzoni mwa msimu inayofuatwa na hali za ukavu zaidi na udongo mwepesi wenye kiasi kidogo cha kaboni.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zilizothibitishwa, zisizo na ugonjwa, na chagua mbegu mbalimbali ili kuongeza ustahimili wa mbegu dhidi ya mnyauko huu usababishwao na Verticillium.
  • Panda mazao mengine kama vile mazao ya nafaka angalau kila baada ya miaka mitatu hadi minne; epuka mazao yanayoathirika kirahisi kama vile viazi, nyanya, pamba, na stroberi.
  • Ondoa mabaki yote ya mazao shambani baada ya kuvuna.
  • Safisha zana za kilimo vizuri kabla ya kuzitumia kwenye shamba lingine.
  • Boresha mtiririko wa maji shambani ili kuepusha hali ya kutuama kwa maji na epuka utumiaji wa mbolea ya nitrojeni kupita kiasi.
  • Dhibiti magugu yaliyopo ndani ya shamba na kwenye eneo linalozunguka shamba.
  • Kagua mazao mara kwa mara, ukizingatia majani na mimea ieneayo upande wa chini, ionyeshayo dalili za hali ya manjano ama hali ya kunyauka.

Pakua Plantix