Waridi

Nyigu

Tenthredinidae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Uharibifu uliotokana na majani ya waridi kuliwa.
  • Majani hugeuka kuwa kama karatasi, hupenyeza mwanga, hukauka, hujikunja na kunyauka.
  • Mmea hupukutika na kudhoofika.
  • Viwavi wadogo, kama konokono, wa rangi ya njano-kijani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Waridi

Waridi

Dalili

Dalili za awali ni mabaka madogo, yanayopitisha mwanga, yaliyo juu ya majani, hivyo jani hubakia na vishipa tu na ganda jembamba, kama karatasi. Kadri jani linavyoendelea kuliwa, maeneo yaliyoharibika hutanuka, hukauka, hugeuka kuwa ya rangi ya kahawia, na husababisha jani kujikunja na kunyauka. Mazaliano mengi yanaweza kumaliza majani yote na kupukutisha mmea. Ingawa mashambulizi madogo kwa kawaida huwa hayaathiri waridi zilizoundwa, mashambulizi yanayojirudia-rudia ama mashambulizi makali huudhoofisha sana mmea, na kuzidisha udhaifu wake dhidi ya visumbufu vingine kama vile wadudu wengine na magonjwa yasababishwao na kuvu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Bidhaa kadhaa zinazokubalika, za viumbe vya kikaboni, zenye kiasi kidogo cha sumu, zinaweza pia kutumiwa moja kwa moja kuuwa kiwavi: sabuni yenye dawa ya kuuwa wadudu huwauwa viwavi wachanga pindi wanapogusana nayo; hakikisha unainyunyizia vizuri katika pande zote za majani. Mafuta ya mwarobaini huvuruga ulaji na ukuaji wa viwavi; nyunyiza mafuta haya mapema asubuhi ama jioni ili kuepuka kuwadhuru wadudu wachavushaji. Dawa ya Spinosad hufyonzwa na tishu za jani na huvuruga mfumo wa neva wa kiwavi pindi kiwavi anapokula jani hilo; ni dawa nzuri lakini inaweza kuathiri vikubwa nyuki na wadudu kadhaa wenye manufaa, hivyo itumie kwa makini. Maadui wa asili, ikiwa ni pamoja na ndege wanaokula wadudu, nyigu wanaonyonya virutubisho kutoka kwa wadudu wengine, mende wawindaji, magonjwa yanayosababishwa na kuvu na virusi, pamoja na wanyama wadogo-wadogo, huifanya idadi ya nyigu hawa kuwa ndogo na wanaweza kusababisha milipuko ya nyigu hawa kupungua. Kuchochea uwepo wa maadui hawa wa asili ndio mbinu bora na endelevu zaidi ya kudhibiti wadudu hawa kwa muda mrefu.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia kwanza kutumia mbinu jumuishi zinazojumuisha mikakati ya kinga sambamba na mbinu za kiasili. Kemikali za kuuwa wadudu zinaweza kuwadhuru wadudu adui wa nyigu hawa na hivyo zinapaswa kutumika tu pale idadi ya kuzaliana kwa wadudu inapokuwa kubwa na pindi njia nyingine zinaposhindwa kufanya kazi. Endapo kama matibabu yanahitajika, chagua bidhaa zinazolenga kuuwa mdudu fulani mahsusi, zilizo na kiasi kidogo cha sumu, badala ya dawa zinazouwa wadudu wengi mbalimbali.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu huu husababishwa na kiwavi cha nyigu wa familia ya Tenthredinidae, ambao hula tishu laini ya majani ya waridi. Nyigu waliokomaa hutumia viungo vyao vinavyofanana na msumeno kupasua sehemu za chini za majani, ambapo hutaga mayai yao. Baada ya mayai kuanguliwa, kiwavi huyu hulila jani kwa takribani wiki nne kabla ya kudondoka ardhini kwa ajili ya kugeuka kuwa pupa. Viumbe hawa waliokomaa ni wanene, kama nyigu, kwa kawaida huwa wa rangi nyeusi au weusi, na jozi mbili za mabawa. Kutegemeana na aina ya spishi, kizazi kimoja hadi vitatu vinaweza kuzaliwa ndani ya mwaka mmoja, huku uharibifu mkubwa zaidi wa shambulizi zao ukishuhudiwa kutokea zaidi kipindi cha majira ya kuchipua na mwanzoni mwa msimu wa kiangazi.


Hatua za Kuzuia

  • Kagua pande zote za majani mara kwa mara, hasa hasa kipindi cha majira ya kuchipua, ili kugundua mazaliano ya wadudu mapema.
  • Ondoa na teketeza majani yaliyoambukizwa, ama waokote viwavi hawa kwa mkono pindi idadi yao inapokuwa ndogo.
  • Wapukutishe viwavi kutoka kwenye mimea kwa kuwapulizia maji kwa kasi; wao hushindwa kupanda juu.
  • Epuka kutumia mbolea za naitrojeni kupita kiasi.
  • Chochea uwepo wa maadui wa asili wa wadudu hawa waharibifu kwa kuotesha mimea yenye nekta nyingi karibu na waridi ili kuwavutia nyigu wanyonyao virutubisho kutoka kwa wadudu wengine, pamoja na wadudu wawindaji.

Pakua Plantix