Vijasidi Warukajani

Karanga

Vijasidi Warukajani

Cicadellidae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Sehemu kavu kwenye majani karibu na maeneo ya ulaji.
  • Maeneo ya manjano kwenye kingo za majani.
  • Wakati mwingine majani yaliyojikunja.
  • Ukuaji uliodumaa.
  • Viruka-majani wenye rangi ya kijani, urefu wa milimita 3-4.

Inaweza pia kupatikana kwenye

22 Mazao
Tufaha
Maharage
Mung'unye
Canola
Zaidi

Vijasidi Warukajani

Karanga

Dalili

Uharibifu unafanana na mwonekano wa mimea yenye uhaba wa majimaji kwenye udongo au upungufu wa virutubisho. Waruka majani hula kwenye upande wa chini wa majani. Majeraha kwa kawaida huanza kwa majani kuwa na maeneo yenye rangi ya manjano yanayokua kuzunguka maeneo ya kula na kujiviriga kidogo kwa kingo za majani. Kwa ujumla, dalili hizi zinajulikana kama "hopperburn". Baadaye, maeneo yenye rangi za manjano huenea kwenye ubapa wote wa jani. Majani yanaweza kujikunja kuelekea chini na hatimaye kudondoka. Hii husababisha ukuaji uliodumaa wa mimea na inaweza kupunguza mavuno ya matunda.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Spinosad na dawa za kuua wadudu za kibaiolojia zenye vimelea vya kuvu kama vile Metarhizium anisopliae, Beauveria bassiana, Paecilomyces fumosoroseus na Verticillium lecanii zinaweza kutumika kudhibiti uvamizi mkali. Sabuni za kuua wadudu pia zinaweza kutumika dhidi ya uvamizi. Kuna wadudu vimelea kama Anagrus atomus ambao wanaweza kutoa njia fulani ya udhibiti. Wadudu wenye manufaa kama vile wadudu-kibibi na mbawakimia ni wawindaji wenye uroho mkubwa wa mayai na lava.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia njia jumuishi zenye hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Matibabu ya mbegu kwa kutumia dawa maalum za kuua wadudu zinazotokana na chlorpyrifos, fipronil au flonicamid yanaonyesha matokeo chanya katika kudhibiti idadi ya wadudu hawa. Dawa hizi zinapowekwa kwenye udongo, zinaua wadudu wanaoishi humo, na hivyo kuwazuia kushambulia mizizi, na pia hutoa ulinzi kwa mmea wenyewe. Matibabu ya kudumu ni pamoja na kupulizia mimea dawa siku 30, 45, 60 baada ya kupanda. Chlorantraniliprole + Lambda-Cyhalothrin (0.5ml/l), Lambda-Cyhalothrin (1ml/l) au Cypermethrin (1ml/l) pia zinaweza kutumika mara 1 au 2 katika hatua za mwisho za ukuaji wa mazao.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na aina kadhaa za waruka majani wa spishi/aina ya Amrasca. Kwa kiasi kikubwa hawa ni wadudu waharibifu wa vitalu nyumba (greenhouses) na hata wakiwa kwa idadi ndogo bado wanaweza kusababisha uharibifu. Vijasidi waruka majani waliokomaa wana rangi ya kijani, wenye urefu/ukubwa wa takriban milimita 3-4, na wakati wa msimu wa baridi huishi kwenye mimea isiyokauka. Majike hutaga mayai yao ndani ya tishu za mishipa ya majani, mara nyingi kwenye upande wa chini wa majani. Lava huanguliwa baada ya wiki moja hadi nne. Tunutu na waruka majani waliokomaa huharibu mimea wanamoishi kwa kunyonya tishu za mimea hiyo. Wakati wakinyonya, wadudu hawa huingiza kemikali zenye sumu ambazo zinaweza kusababisha kuziba kwa mishipa ya mmea, ndiyo maana dalili zake zinafanana na upungufu wa maji au virutubisho.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha unapata mimea yenye afya, kwani waruka majani wanaofanana na panzi hutokea kwa urahisi kama mayai yaliyofichwa ndani ya tishu za mimea.
  • Tumia aina za mimea zinazostahimili zaidi kuliwa na wadudu.
  • Kagua majani ili kugundua uwepo wa ngozi tupu za tunutu (panzi/waruka jani wachanga) kwenye upande wa chini wa majani.
  • Chuma kwa mkono na ondoa mayai au sehemu za mimea zilizoathirika.
  • Vinginevyo, tumia mitego ya kunata ya rangi ya manjano ambayo huwavutia sana waruka majani wa kijani.
  • Dhibiti matumizi ya dawa za kuua wadudu kwani dawa hizi zinaweza pia kuathiri wadudu wenye manufaa(kama vile wadudu wanaokula wadudu waharibifu).
  • Jaribu kuendeleza mazingira mazuri yanayoweza kuwavutia wadudu wenye manufaa kama vile wadudu-kibibi na mbawakimia.

Pakua Plantix