Phytophthora colocasiae
Kuvu
Dalili za mwanzo ni madoa madogo ya rangi ya kahawia, yenye kingo zilizolowa maji, na yalizozungukwa na mwangaza wa njano. Madoa haya hutokea maeneo ambayo maji hujikusanya kwenye jani. Huanza kidogo kidogo lakini hukua upesi sana kuwa madoa makubwa ya mviringo, ya rangi ya kahawia, ambayo huweza kufunika zaidi ya nusu ya jani. Moja ya dalili ya kipekee ya ugonjwa huu ni majimaji ya rangi ya machungwa au rangi nyekundu ambayo humiminika kutoka kwenye maeneo yenye maambukizi. Majimaji haya ni rahisi kuonekana katika eneo la chini ya majani. Wakati wa mchana, majimaji haya hukauka na kuwa gamba gumu la rangi ya kahawia iliyokolea. Kadri ukubwa wa madoa unavyozidi kuongezeka, madoa haya huharibu sehemu yote ya majani. Majani yanaweza pia kuwa na vishimo vifupi vilivyozungukwa na ungaunga mweupe ulio katika muundo wa pete. Shina za majani hupata vidonda vya rangi ya nyekundu-kahawia. Ugonjwa huu unapofika kwenye mizizi iliyo chini ya ardhi, mizizi hii hugeuka kuwa migumu na ya rangi ya kahawia, hata hivyo, huoza haraka punde baada ya kuvunwa.
Spishi za Trichoderma zimeonyesha kuwa nyenzo fanisi zaidi ya udhibiti wa kiasili. Chovya miche kwenye tope la Trichoderma kabla ya kuiotesha. Andaa ziduo la mmea katika ukolevu wa 10-20 mg/ml. Tumia mbinu hii kama njia ya kukinga maambukizi, kabla ya ugonjwa kuibuka. Tibu mimea utakayootesha kwa kutumia nyenzo za kiasili za kudhibiti maambukizi kabla ya kuotesha mimea hiyo. Jumuisha matumizi ya mbinu mbalimbali za kiasili ili kupata matokeo bora zaidi.
Udhibiti wa kemikali mara nyingi si mbinu inayotumika katika kudhibiti bakajani la gimbi. Mvua za mara kwa mara huondoa dawa ya kuuwa kuvu haraka, hivyo kusababisha gharama za kufanya matibabu tena na tena, jambo ambalo si fanisi. Kutumia aina mbalimbali za bidhaa kinzani ni bora zaidi kuliko kunyunyiza kemikali. Tumia dawa za kuuwa wadudu zilizothibitishwa kama njia ya kuzuia maambukizi, kabla dalili za ugonjwa hazijajitokeza. Anza kunyunyiza dawa pindi hali ya hewa inapoonekana kuwa rafiki kwa uibukaji wa ugonjwa huu. Nyunyiza tena kila baada ya mvua kubwa kunyesha, kama ikiwezekana. Jizatiti katika kunyunyizia sehemu yote ya chini ya majani ambapo maambikizi huanzia. Tumia vinyunyizi vyenye ujazo mkubwa ili kunyunyizia eneo lote vizuri. Zingatia unafuu wa gharama - inaweza isiwe ya gharama nafuu kwa mashamba madogo madogo.
Bakajani la Gimbi husababishwa na Phytophthora colocasiae, kuvu wa maji ambaye hustawi katika hali za unyevunyevu. Pathojeni huyu husambaa kutoka mmea mmoja kwenda mwengine kupitia rasha-rasha za mvua na katika mvua inayopeperushwa na upepo. Viini vidogo huanguka kwenye majani na shina ambapo huchipua haraka wakati wa hali ya hewa ya unyevunyevu. Katika mashamba ya magimbi yaliyofurikwa na maji, ugonjwa huu husambaa haraka zaidi kupitia maji yaliyopo shambani, ambayo hupeleka viini kwenye mimea yenye afya. Ugonjwa huu hupendelea hali ya hewa ya mvua na ya joto. Husambaa upesi zaidi pindi unyevunyevu wa hewa unapozidi kiwango cha 90% na pindi halijoto inapofikia 30°C. Pathojeni huyu anaweza kuishi kwenye tishu za mmea na kwenye udongo, hivyo ni ngumu kumtokomeza pindi anapoingia shambani. Pia anaweza kuishi kwenye mizizi iliyoambukizwa kipindi cha wakati usio wa msimu na kisha kuanza maambukizi mapya pindi unapoiotesha mizizi hiyo. Tofauti na magimbi, ugonjwa huu hushambulia pia dasheen na mimea kadhaa mengine inayoweza kuwa chanzo za maambukizi. Bakajani la gimbi ndio ugonjwa haribifu zaidi wa magimbi ulimwenguni kote.

This page is powered by millions of live Plantix diagnoses. See where Bakajani la Magimbi is spreading — district by district — with Crop Insights, part of Plantix Intelligence.