Karoti

Baka la Karoti

Alternaria dauci

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Madoa ya rangi ya kahawia iliyokolea hadi nyeusi katika ncha na kingo za majani.
  • Majani huonekana yamenyauka na kuwa na mabaka.
  • Majani ya chini, yaliyokomaa, huathirika kwanza.
  • Vikonyo vinaweza kukandamizwa na kuuliwa, majani huanguka.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao
Karoti

Karoti

Dalili

Dalili za awali kabisa za maambukizi huonekana kama vidonda vidogo, visivyo vya kawaida, vya rangi ya kahawia iliyokolea hadi nyeusi, kwenye kingo na ncha za majani yaliyokomaa, yaliyopo kwenye ukanda wa chini. Vidonda hivi vinaweza kuwa na ukubwa mbalimbali na vinaweza kuzungukwa na duara la njano. Baada ya muda, madoa haya hupanuka na kuungana na mengine, hivyo kulifanya jani kuwa na mwonekano wa baka lililoungua. Majani yaliyoathiriwa sana hunyauka na kufa. Katika hatua za baadae, vidonda vikubwa vinaweza pia kujiunda kwenye vikonyo, wakati mwengine huvikandamiza kabisa na kusababisha majani kudondoka. Wakati mwengine, pathojeni huyu huathiri miche michanga iliyopo ardhini ama chini kidogo ya udongo, hivyo kusababisha miche kunyauka. Vikonyo vyenye maambukizi huvunjika kwa urahisi wakati wa mavuno, jambo linaloweza kusababisha mizizi kuachwa ndani ya udongo.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Tumia kinga kutibu kuvu huyu. Bidhaa zenye madini ya shaba zimeonyesha kuwa na athari fulani katika ugonjwa huu, na tafiti kadhaa zimetaja spishi za Trichoderma na Bacillus kama spishi zinazoweza kupambana na kuvu huyu. Kama ilivyo katika mbinu nyingine zote za kiasili, ufanisi unaweza kutofautiana kutegemeana na aina ya karoti na hali za kimazingira. Daima zingatia kujumuisha matibabu ya kiasili na mbinu za kitamaduni na za kinga, ili kupata matokeo bora zaidi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia kutumia mbinu jumuishi zinazojumuisha mikakati ya kinga sambamba na matibabu ya kiasili, kama ikiwezekana. Matumizi ya dawa za kuuwa kuvu yanapaswa kuanza pindi dalili za kwanza zinapogundulika, ama kama kinga katika kanda zenye unyevunyevu ambapo ugonjwa huu huibuka mara kwa mara. Kadri kanopi inavyojifunga, kanopi huwa ngumu zaidi kunyunyiziwa dawa vizuri, hivyo basi, unyunyiziaji dawa mapema huwa fanisi zaidi. Badili aina ya dawa ya kuuwa kuvu ili kupunguza hatari ya mmea kugeuka kuwa sugu. Bidhaa zenye madini ya shaba zinaweza pia kutumika badala ya dawa za kuuwa kuvu, na zimeonyesha kuweza kutokomeza baka la jani la Alternaria, na huenda pia zikasaidia kukomesha baka la jani linalosababishwa na bakteria.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huu husababishwa na kuvu Alternaria dauci, anayeweza kusambazwa kupitia mbegu zilizoathiriwa ama zilizo na maambukizi, na anaweza kujihifadhi kwenye mabaki ya mimea na kwenye mimea ya karoti kipindi cha msimu wa baridi. Kuvu huyu hawezi kuishi kwenye udongo bila kuwepo kwa mmea ulio hai. Viini vya kuvu huyu husambazwa na upepo na kurushwa-rushwa na mvua ama umwagiliaji wa juu ya mmea hadi kuifikia mimea iliyopo jirani, na vinaweza kubebwa umbali mrefu na upepo na kwenye vifaa vya shamba. Maambukizi hushamiri zaidi katika hali ya hewa ya joto (16-35°C) na katika vipindi virefu vya unyevunyevu wa majani. Kwa kawaida, ni masaa 8 hadi 12 tu ya unyevunyevu kwenye majani ndio huhitajika ili viini hivi viweze kuchipua na kuambukiza mmea. Kadri halijoto inavyoongezeka, kipindi cha unyevunyevu kinachohitajika kusababisha maambukizi hupungua. Makali ya ugonjwa huwa juu zaidi katika mimea iliyodhoofika, isiyo na mbolea ya kutosha.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia mbegu zilizothibitishwa, zisizo na maambukizi, na zenye ukinzani mkubwa dhidi ya ugonjwa huu, pale inapowezekana.
  • Acha nafasi kubwa baina ya mmea na mmea, na inua safu za mimea ili kuboresha mzunguko wa hewa na kupunguza muda wa unyevunyevu kwenye majani.
  • Epuka umwagiliaji wa juu ya mimea; kama ikishindikana, mwagilia wakati wa mchana ili majani yaweze kukauka haraka.
  • Weka mbolea ya kutosha.
  • Vuna wakati sahihi na changanya upesi mabaki ya mazao kwenye udongo baada ya kuvuna.
  • Otesha mazao tofauti kwa kipindi cha angalau miaka miwili ili kupunguza hatari ya kuibuka kwa ugonjwa huu.

Pakua Plantix