Kuongoza mabadiliko ya kidijitali kwenye kilimo ili kuinua kilimo kilicho endelevu kimazingira na kiuchumi.
Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, Plantix imejiimarisha kama mtaalamu wa kidigitali wa ubainishaji wa magonjwa ya mimea na kilimo. Leo, tunawaunganisha wakulima wadogo na wasambazaji katika mfumo mmoja wa kidijitali kupitia programu zetu mbili, Plantix na Plantix Partner. Malengo yetu ya msingi ni pamoja na kutoa masuluhisho binafsi, bidhaa za kuaminika na huduma zinazoaminika. Tayari tumekwishajibu mamilioni ya maswali yanayohusu kilimo na mazao kutoka kwa wakulima na kuunganishwa kidijitali na mamia ya maelfu ya wauzaji reja reja.
Suluhu zilizobinafsishwa, bidhaa za kuaminika na huduma zinazoaminika ndio malengo yetu makuu. Mwaka jana, tulijibu zaidi ya maswali milioni 50 yanayohusiana na kilimo na mazao kutoka kwa wakulima, na tuliunganisha kidijitali zaidi ya wauzaji rejareja 100,000.
watumiaji 134,000 wa programu kila siku
Ubainishaji wa ugonjwa 1 kila sekunde 1,5
Inapatikana katika nchi 177 na lugha 18
Uwasilishaji wa chapa zaidi ya 40 na zaidi ya bidhaa 1000
Inafanya kazi katika majimbo 10 ya India
Inaaminiwa na wafanyabiashara rejareja zaidi ya 100,000
250+ Wafanyakazi wa Plantix
Makao Makuu yanapatikana:
Berlin · Indore
Kama afisa mtendaji mkuu (Mkurugenzi Mtendaji) na mwanzilishi mwenza, Simone Strey anaisukuma Plantix kuyafikia maono ya kuongoza mabadiliko ya kidijitali katika kilimo ili kuinua kilimo kilicho endelevu kimazingira na kiuchumi.
Simone ana Shahada ya Uzamili ya Jiografia kutoka Chuo Kikuu cha Leibniz Hanover. Kazi yake ilimtoa kutoka Berlin, Msitu wa Mvua wa Amazon, hadi kufika Afrika Magharibi, Gambia na India, ambako alipata uzoefu wa moja kwa moja na uelewa wa mahitaji ya wakulima wadogo.
Simone pia alifanikiwa kuanzisha asasi isiyo ya kiserikali ya 'Green Desert eV', ili kutengeneza masuluhisho ya kiufundi yanayojitosheleza katika miundombinu ya maji, kilimo na nishati.
Robert Strey, afisa mkuu wa teknolojia wa Plantix (CTO) na mwanzilishi mwenza, ni mbunifu wa teknolojia ya kisasa ya Plantix na hifadhidata ya kilimo. Robert ana Shahada ya Uzamili ya Jiografia kutoka Chuo Kikuu cha Leibniz Hanover.
Lengo lake kuu katika Plantix ni kuimarisha mkakati wa kampuni wa kutumia rasilimali za kiteknolojia zilizo bora, zenye faida na zilizo salama,pamoja na kutekeleza mifumo mipya ya miundombinu.
Kwa maswali yote ya habari, tafadhali tutumie barua pepe kwenda:
press@plantix.net