Nyanya

Uvimbe wa Majani

Transpiration disorder

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Malengelenge/uvimbe kwenye majani, shina na matunda.
  • Majani yaliyokakamaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Nyanya

Dalili

Malengelenge/Viupele vyenye maji na madoa ya njano kwenye upande wa chini wa majani. Hii inaweza kusababisha kujikunja kusiko kwa kawaida kwa majani. Malengelenge hayo yanaweza kutokea kwenye shina na matunda pia. Majani yanaweza kukakamaa na yanaweza kupasuka yanapoguswa. Hii ni kwa sababu malengelenge hudhoofisha muundo wa majani. Ingawa uvimbe wa majani kwa kawaida hauathiri afya ya mmea kwa ujumla, inaweza kufanya mboga isiwe na mvuto sana kwa kuuza, na hivyo kusababisha hasara za kiuchumi. Sehemu zote laini za mazao ya mboga mboga zinaweza kuupata uvimbe wa majani ikiwa hali ya hewa inaruhusu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

JAMBO hili si mdudu wala ugonjwa; kwa hivyo, udhibiti wa kibayolojia hauhitajiki au hauhusiki.

Udhibiti wa Kemikali

Jambo hili si mdudu wala si ugonjwa; kwa hiyo, udhibiti wa kikemikali hauhitajiki au hauhusiki.

Ni nini kilisababisha?

Kumwagilia kupita kiasi, udongo unao tuamisha maji, siku za baridi na mawingu, unyevu mwingi. Uvimbe wa majani hutokea wakati mimea inafyonza maji kwa kasi zaidi kuliko inavyoweza kuyatoa kupitia majani. Mara nyingi hutokana na kumwagilia kupita kiasi siku za mawingu na mwanga hafifu, unyevu wa juu au mzunguko mdogo wa hewa. Kabichi na nyanya huathiriwa sana na hali hii, hasa katika udongo unao tuamisha maji. Malengelenge yanayosababishwa na uvimbe wa majani huendelea kuwepo hata kama hali ya hewa inapo boreka.


Hatua za Kuzuia

  • Epuka kumwagilia maji kupita kiasi, hasa kipindi chaa baridi na mawingu wakati ambapo mimea inapaswa kuwa na ukavu kiasi.
  • Ongeza sehemu za kuingizia hewa na kuepuka msongamano wa mimea ili kuboresha mzunguko wa hewa.
  • Punguza kumwagilia wakati wa hali ya hewa inayo chochea Uvimbe wa Majani lakini usiruhusu mimea kuwa kwenye ukavu kabisa.
  • Mwagilia kila wakati asubuhi tu.
  • Epuka kutumia mbolea kupita kiasi, haswa wakati wa ukuaji wa polepole.
  • Kuwa mak ini na viwango vya potasiamu na kalsiamu kwenye udongo, kwani elementi hizi husaidia uthabiti wa tishu za mimea.
  • Baadhi ya aina za mimea zinaweza kuwa sugu/kinzani zaidi kwa Uvimbe wa Majani.

Pakua Plantix