Kiazi

Kubadilika Rangi ya Kiazi

Anthocyanin pigmentation

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Kubadilika kwa rangi kuwa pinki ndani ya tunguu la kiazi.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Kiazi

Dalili

Eneo la rangi ya pinki au zambarau linalofanana na mduara au madoa ndani ya tunguu la viazi. Rangi ya pinki inaweza kutofautiana katika uangavu. Wakati mwingine mabadiliko ya rangi huenea hadi ndani kabisa. Aina zingine za viazi zilizo na ngozi ya manjano zinaweza kuonyesha rangi ya pinki kwa nje pia.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Suala hili si mdudu wala ugonjwa; kwa hiyo, udhibiti wa kibaiojia hauhitajiki au siyo muhimu.

Udhibiti wa Kemikali

Suala hili si mdudu wala ugonjwa; kwa hiyo, udhibiti wa kemikali hauhitajiki au siyo muhimu. Mara tu dalili hizi zinapo onekana kwenye mmea, hazidumu.

Ni nini kilisababisha?

Mabadiliko ya rangi ya pinki katika tunguu la viazi, inayojulikana kama anthocyanin pigmentation, inaweza kutokea kwa sababu kadhaa. Katika aina fulani rangi hii ya pinki inaonekana wakati viazi vimeambukizwa na virusi vya kukunja majani ya viazi mviribgo. Rangi hii pia inaweza kuathiriwa na hali za kimazingira. Kwa mfano, kuwekwa wazi kwenye mwanga, hasa kwa viazi karibu na ardhi, mfululizo wa usiku wa baridi na kutwa za joto, au kukua katika udongo mkavu au wenye naitrojeni nyingi.


Hatua za Kuzuia

  • Ili kupunguza rangi ya waridi/pinki kwenye tunguu la viazi, jenga matuta makubwa ambayo yanaweza kupunguza kubadilika rangi kwa nyama ya kiazi.
  • Hakikisha umwagiliaji wa mara kwa mara lakini epuka kumwagilia kupita kiasi.
  • Zaidi ya hayo, zuia viazi kupata mwanga wa jua la mchana isipokuwa wakati wa shughuli muhimu kama vile kuvuna, kuhifadhi, na kufungasha, na punguza mwangaza wa jua wa moja kwa moja iwezekanavyo.

Pakua Plantix