Thermal stress
Nyingine
Dalili za mfadhaiko/msongo wa joto kwenye mpunga zinaweza kutofautiana kulingana na hatua ya mpunga. Mapema, unaweza kusababisha miche kufa, na maotea machache (mashina ya kuchipua kutoka kwenye shina kuu). Majani yanaweza kuanza kujikunja na kuonekana yameungua. Wakati wa kuchanua, makundi ya vishada/masuke yanaweza kugeuka kuwa meupe na kuonekana yamesinyaa, kuonyesha chavua dhaifu. Wakati punje za mpunga zinatengenezwa, joto linaweza kusababisha maendeleo yasiyo kamili. Madhara makuu ni kwamba mfadhaiko wa joto hupunguza kiwango na ubora wa mchele uliovunwa.
Suala hili si mdudu wala ugonjwa; kwa hiyo, udhibiti wa kibaiolojia hauhitajiki au siyo muhimu.
Suala hili si mdudu wala ugonjwa; kwa hiyo, udhibiti wa kemikali hauhitajiki au hauhusiki.
Aina hii ya mfadhaiko hutokea wakati halijoto inapozidi kiwango kile ambacho mmea unahitaji kukua, na kuzaliana ipasavyo. Wakati joto la mchana na usiku linaweza kusababisha mfadhaiko wa joto, athari ni mbaya zaidi usiku kuliko wakati wa mchana. Mabadiliko ya tabia ya nchi yanaonekana kuwa sababu kuu ya suala hili kuwa la kawaida zaidi kwa sasa. Ni muhimu kukumbuka kuwa joto jingi na ukosefu wa maji unaweza kusababisha tatizo hili.