Pamba

Muunguzo wa Viua Magugu

Herbicides Cell Membrane Disruptors

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Madoa ya majani yaliyotota maji.
  • Majani kunyauka na kuwa ya kahawia.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Pamba

Dalili

Dalili zinategemea na dawa ya kuua magugu iliyotumika, wakati ilipotumika, na dozi yake. Kwa ujumla, majani huonesha vidonda vilivyotota maji, ambavyo baadaye hukauka. Kuungua kwa tishu au kushindwa kuchipua ni tabia ya dawa hizi za kuua magugu pale zinapotumika kabla ya kuota. Zinapotumika baada ya kuota, zinaweza kusababisha kuungua kwenye muundo au mpangilio wa madoa. Inaweza kuchanganywa kwa kufananishwa na majeraha yanayotokana na dawa za kuua magugu za paraquat lakini haina rangi ya shaba.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna matibabu ya kibaolojia yanayopatikana kwa ajili ya tatizo hili. Kinga na mbinu bora za kilimo ndizo njia muhimu za kuepuka madhara yanayoweza kutokea. Osha na suuza mimea vizuri ikiwa kuna mashaka ya kutumia dozi kubwa kupita kiasi.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga na matibabu ya kibaolojia, ikiwa yanapatikana. Kabla ya kupanga kupulizia dawa ya kuua magugu, hakikisha unajua aina ya magugu unayokabiliana nayo (kimsingi magugu yenye majani mapana dhidi ya nyasi) na chagua mbinu bora zilizopo. Chagua dawa ya kuua magugu kwa uangalifu na fuata maelekezo ya dozi kama ilivyoonyeshwa kwenye lebo.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na dawa za kudhibiti magugu za vizuizi PPO, zikiwemo Flumioxazin, Fomesafen, Lactofen, Carfentrazone, na Acifluorfen, ambazo ni za familia ya diphenyl ether. Pamoja na mengine, dawa hizi zinavuruga utando wa seli kwa kuzuia uzalishaji wa klorofili. Dalili kwenye majani huonekana ndani ya siku 1-3, kutegemea na mwanga na hali ya hewa. Dalili hizi huchochewa na mwanga na huwa mbaya zaidi katika siku zenye mwanga mkali na joto.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha unafahamu aina ya magugu unayoshughulika nayo (kwa kawaida magugu yenye majani mapana au nyasi).
  • Chagua kwa umakini dawa ya kuua magugu inayokidhi zaidi kwa malengo yako.
  • Soma lebo kwa umakini na fuata maelekezo ya dozi kama yalivyooneyeshwa kwenye lebo.
  • Daima safisha chombo unachotumia kupulizia dawa baada ya matumizi ili kuepuka uchafuzi na dawa nyingine ya kuua magugu.
  • Epuka kupulizia dawa wakati wa upepo ili kuzuia kuperurushwa kwa dawa hadi kwenye mashamba mengine.
  • Tumia nozeli ya kupunguza upeperushwaji wa dawa ambayo inalenga magugu vizuri zaidi.
  • Jaribu kutumia dawa ya kuua magugu kwenye malisho na mashamba ya majani makavu ili kuchunguza ufanisi wake.
  • Fuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa umakini na usipulizie wakati wa hali ya jua na joto.
  • Hifadhi kumbukumbu ya shughuli za shamba zikiwa na tarehe za kupulizia dawa, aina ya madawa, maeneo ya shamba na hali ya hewa.

Pakua Plantix