Herbicides Growth Regulators
Nyingine
Dalili huonekana zaidi kwenye majani machanga, yanayokua. Tabia zinazobainisha uwepo wa ugonjwa ni ubapa wa majani kukunjika, kupinda au kujisokota. Mashina na vikonyo hujisokota na kujipinda pinda. Malengelenge hujitokeza kwenye uso wa majani, na hivyo kufanya majani yaonekane yaliyorefuka au kuwa na umbo mithili ya mikono ya wachawi. Kutokana na majani kupoteza umbo lake la asili, mishipa ya majani huonekana kama inayoelekea upande mmoja (sambamba) badala ya kukatizana mithili ya nyavu. Rangi ya majani hubadilika kutoka kuwa ya manjano hadi nyeupe na kahawia. Hakuna uharibifu unaotokea kwenye sehemu za mimea iliyokomaa kama vile majani ya zamani au vitumba vilivyokua.
Hakuna matibabu ya kibaiolojia yanayopatikana kwa tatizo hili. Kuzuia/kukinga na mbinu bora za kilimo ndiyo njia kuu za kuepusha madhara kutokea tangu mwanzo. Endapo unashuku kuwa kipimo cha dawa kilikuwa kikubwa zaidi, inaweza kusaidia endapo utaosha au kusuuza mimea kwa ukamilifu.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Kuzuia na mbinu bora za kilimo ndiyo njia kuu za kuepuka madhara kutokea tangu mwanzo. Kabla ya kupanga kupulizia dawa ya kuua magugu, hakikisha unajua aina ya magugu unayokabiliana nayo (kimsingi magugu yenye majani mapana dhidi ya nyasi) na chagua mbinu iliyo bora zaidi. Chagua kwa uangalifu dawa ya kuua magugu na fuata maagizo ya kipimo kama yalivyoonyeshwa kwenye lebo.
Dalili hujitokeza ndani ya siku chache baada ya matumizi ya dawa za kuua magugu zinazotokana na kundi la phenoxyacetic acids or synthetic auxins (kundi I). Mimea ya pamba huathirika kirahisi sana kwa dawa za kuua magugu za aina ya 2,4-D au dicamba, ambazo hutumika kudhibiti magugu yenye majani mapana. Utumiaji wa dawa hizi katika muda usio muafaka, uchaguzi usio sahihi wa mchanganyiko wa madawa au hali mbaya ya hewa, yote hayo yanaweza kusababisha dalili zilizoelezwa kwenye mimea ya pamba. Uchafuzi pia unaweza kusababishwa na mashamba yaliyo jirani. Mimea inayokabiliwa na hali isiyo rafiki kwa ukuaji huwa na uwezekano mkubwa wa kuathirika. Usambaaji wa dalili hutegemea na kipimo/dozi cha dawa na unaweza kuanzia kwenye vifundo vichache hadi mmea mzima ikiwa kiwango ni cha juu sana. Ni muhimu kuelewa kwamba dawa za kuua magugu zinaweza kuharibu mazao hata kwa dozi ndogo.