Parawilt
Nyingine
Parawilt, pia hujulikana kama mnyauko wa ghafla, hutokea kwa nadra katika mashamba na kwa wakati usiojulikana. Hakuna mpangilio halisi wa shamba unaohusiana na tatizo hili na mara nyingi hufananishwa kimakosa na magonjwa yanayosababishwa na vimelea vya magonjwa. Dalili kuu ni kunyauka na kubadilika kwa rangi ya majani. Rangi ya majani inaweza kubadilika kutoka rangi ya manjano hadi ya shaba au nyekundu, na baadaye kufuatiwa na kukauka kwa tishu. Tatizo hili huathiri hasa mimea yenye ukuaji wa haraka, majani mengi, na mzigo mzito wa vitumba vya pamba. Kupukutika mapema kwa vitumba vya pamba na majani na kufunguka mapema kwa vitumba kunaweza kutokea. Mimea inaweza kupona lakini mavuno yataathiriwa vibaya.
Hakuna hatua za udhibiti wa kibaiolojia kwa parawilt au mnyauko wa ghafla. Ili kuepuka tatizo hili, ni muhimu kurekebisha umwagiliaji na utumiaji wa mbolea kwenye mimea ya pamba na kupangilia mfumo mzuri utoaji maji kwenye udongo.
Daima fikiria kutumia mbinu jumuishi pamoja na hatua za kinga na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna matibabu ya kikemikali ya kutibu tatizo hili. Hata hivyo, unaweza kuanza kwa kuondoa maji ya ziada kupitia mifereji ya maji. Andaa mchanganyiko wa gramu 15 za urea, gramu 15g za muriate ya potash, na gramu 2 za copper oxychloride katika lita 1 ya maji. Ongeza mililita 100-150 za maji karibu na eneo la mizizi ya mmea. Mchanganyiko huu hutoa virutubisho vya papo hapo kwa mmea na dawa za kuua kuvu huzuia maambukizi ya kuvu.
Parawilt ni tatizo la kimaumbile, ikiwa na maana ni tatizo ambalo halisababishwi na kuvu, bakteria, virusi au vijidudu vingine sawa na hivyo. Tofauti na magonjwa mengine au dhiki zinazosababisha dalili zinazofanana na tatizo hili kwenye mimea ya pamba, parawilt hujitokeza ndani ya saa chache tu bila ya muundo maalum wa kieneo. Usambaaji wa hapa na pale na kutokea kwa tatizo katika wakati usio muafaka ni dalili za kawaida za parawilt. Hivi sasa inajulikana kwamba tatizo hili linatokana na mkusanyiko wa ghafla wa maji karibu na mizizi (baada ya mvua kubwa au umwagiliaji kupita kiasi) kisha kufuatiwa na joto kali na mwanga mkali wa jua. Ukuaji wa haraka wa mimea na uwiano usio sahihi wa virutubisho pia ni miongoni mwa vyanzo vya tatizo hili. Udongo wenye kiwango kikubwa cha udongo wa mfinyanzi au udongo usiopitisha maji vizuri huongeza uwezekano wa mimea kupata tatizo hili.