Pamba

Wekundu wa Jani la Pamba

Leaf Reddening

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Kingo za majani zinageuka kuwa nyekundu kwanza, kisha kubadilika rangi kwa jani lote.
  • Mashina kunyauka na kuwa mekundu.
  • Majani na matunda kuanguka.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Pamba

Dalili

Kugeuka kwa rangi ya majani na kuwa mekundu kunaweza kutofautiana kidogo kulingana na sababu na hatua ya ukuaji wa mmea. Mara nyingi, kingo za majani hugeuka kuwa nyekundu kwanza na baadae kubadilika kwa rangi ya jani kutaenea kwenye sehemu nyingine ya jani. Dalili nyingine zinaweza kuwa ni pamoja na kunyauka, mashina kuwa mekundu, kuwa na vitumba dhaifu au kutokuwepo kabisa, kudondoka kwa majani na matunda, na kudumaa ukuaji wa mimea. Wakati wa uzeekaji wa mmea, ubadilikaji rangi wa majani ni mchakato wa kawaida ambao unaweza kuonekana katika shamba lote. Mbali na upungufu wa naitrojeni, majani kubadilika rangi na kuwa mekundu kunaweza pia kusababishwa na mwanga wa jua unaopiga moja kwa moja kwenye majani, baridi, na uharibifu unaofanywa na upepo. Katika hali hiyo, kubadilika rangi huathiri majani machache badala ya shamba lote.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kutegemea na mfadhaiko (mimea kukua katika mazingira yasiyo muafaka) na hatua ya ukuaji, matumizi ya mbolea za kikaboni yanaweza kuwa na manufaa kwa mimea. Udhibiti wa kibaiolojia hauna umuhimu ikiwa wekundu wa majani unaanza kutokea mwishoni mwa msimu au ikiwa mchakato huo unasababishwa na sababu za kiasili.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kukinga na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Hakuna udhibiti wa kemikali unaopatikana kwa ajili ya kudhibiti majani ya pamba kubadilika na kuwa mekundu. Uwekaji mzuri wa mbolea ya samadi, mpango wa umwagiliaji unaozingatia matumizi sahihi ya maji, na utumiaji wa mbolea zenye uwiano sahihi kutasaidia kuepuka tatizo tajwa. Ikiwa inatokea mwanzoni mwa msimu, marekebisho ya virutubisho yanaweza kusaidia kutatua tatizo la wekundu kwenye majani. Ikiwa dalili zinaanza karibu na muda ule ule wa vitumba vya awali kufunguka, hakuna hatua zinazohitajika kuchukuliwa.

Ni nini kilisababisha?

Dalili zinaweza kusababishwa na mambo mbalimbali za kimazingira kama vile maji, athari ya joto endelevu, au udongo wenye rutuba duni. Baadhi ya aina ya mimea au mimea chotara inaweza kuwa na athari zaidi kuliko zingine. Kuwa na wekundu kunasababishwa na kuongezeka kwa pigmenti (kiwango cha rangi ya asili) nyekundu iitwayo anthocyanin na kupungua kwa umbijani (klorofili) ya pigmenti ya kijani kwenye majani. Sababu inaweza kuwa kufa kwa mizizi midogo na hivyo kupunguza uwezo wa mmea kunyonya maji na virutubisho kwa ufanisi. Wakati wa uzeekaji wa mimea, mchakato huu ni wa kawaida na hauna athari mbaya kwa mavuno. Sababu zingine mapema mwa msimu zinaweza kuwa upungufu wa naitrojeni, fosforasi, na potasiamu (magnesi/magneziamu haionekani kuhusika). Zaidi ya hayo, mimea kuanikwa wazi moja kwa moja kwenye mwanga wa jua, upepo na baridi, pia inaweza kusababisha kubadilika kwa rangi.


Hatua za Kuzuia

  • Panda kwa wakati unaopendekezwa ili kuepuka joto kali la udongo wakati wa kuzaa matunda.
  • Angalia umbali bora (muafaka) kati ya mimea.
  • Tumia aina za pamba zinazostahimili athari za kimazingira (kwa mfano, athari zinazotokana na upepo mkali, jua kali, ukame, n.k).
  • Hakikisha unatia mbolea ya samadi ya kutosha kwenye udongo.
  • Linda mazao dhidi ya mfadhaiko wa kimaumbile kama vile uharibifu wa moja kwa moja unaotokana na upepo.
  • Panga umwagiliaji unaozingatia matumizi sahihi ya maji na kwa uangalifu kwa kuangalia mahitaji ya mimea.
  • Fuatilia virutubisho vya udongo na tumia mbinu za usimamizi wa virutubisho kwa uwiano sahihi.
  • Baada ya mavuno lima kwa kuchimbua udongo ili kuuchanganya.

Pakua Plantix