Nyanya

Ugonjwa wa Mikunjo ya Nyanya

Fruit Deformation

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Nyufa za mzunguko huonekana kwenye matunda na tabaka la juu la ngozi ya tunda huanza kuwa na mwonekano wa kijivu.
  • Kasoro hii husababishwa hasa na matatizo ya maji au unyevunyevu.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Nyanya

Dalili

Nyufa ndogo ndogo, nyingi, zinazofanana na nywele zinaonekana kwenye ngozi ya nyanya, mara nyingi hufuata muundo wa mzunguko. Tabaka la juu la ngozi ya tunda huanza kuwa na mwonekano wa kijivu. Nyufa hizo huwa na urefu wa milimita chache na kwa kawaida huanza kuonekana mwanzoni mwa kukomaa. Matunda ambayo yameathiriwa moja kwa moja na kiasi kikubwa cha dawa za kuua wadudu yana uwezekano mkubwa wa kupata vidonda vya aina hii. Dawa ya kuua wadudu huunguza unyumbufu wa ngozi ya ndani na kupelekea mipasuko.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna matibabu ya kibaolojia yanayopatikana kwa ugonjwa huu. Unaweza kutibiwa tu na hatua za kuzuia.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ugonjwa huu unaweza kutibiwa tu na hatua za kuzuia, uharibifu hauwezi kurekebishwa. Hata hivyo, epuka matumizi mengi na mchanganyiko wa dawa za kuua wadudu ili kuepuka dalili za ugonjwa huu.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa huu wa kimaumbile unaweza kufanana na nyufa za ukuaji, ingawa alama zinazosababishwa na russeti ni ndogo zaidi, fupi na za juu juu. Mara nyingi huhusishwa na mazingira ya kitalu nyumba yenye unyevunyevu na mabadiliko ya unyevu wa udongo na joto la mchana/usiku. Viwango visivyofaa vya maji (ukame, mabadiliko katika kumwagilia/mvua, mafuriko), ziada/upungufu wa virutubisho na mwangaza pia unaweza kuwa sababu. Hatimaye matumizi mabaya au makubwa ya viua wadudu yanaweza kuzidisha hali hiyo. Matunda huwa katika hatari zaidi kwa vile yanakua kwenye ncha za ukuaji na inatakiwa yashindane na machipukizi mapya kupata maji na virutubisho.


Hatua za Kuzuia

  • Kuwa mwangalifu na matibabu ya dawa na epuka matumizi kupita kiasi na mchanganyiko wa dawa tofauti.
  • Hakikisha mimea yako ina kifuniko cha kutosha cha majani ili kulinda matunda.
  • Weka matandazo ya kutosha katika hali ya hewa ya joto ili kuweka udongo kuwa baridi na kupunguza uvukizi.
  • Zingatia kitalu kilichoinuliwa kwa upitishaji maji bora kwenye udongo.
  • Mwagilia katikati ya asubuhi na sio wakati wa jua kali la mchana.
  • Tumia nyenzo za kivuli ili kupoza mimea yote.
  • Chuma nyanya mapema wakati matunda yanaonyesha rangi.

Pakua Plantix