Fruit Deformation
Nyingine
Dalili huonekana kwa namna ya nyufa na kupasuka kwa ngozi ya nje ya matunda. Kina na ukubwa wa mipasuko na nyufa vinaweza kutofautiana na kwa kawaida hutokea karibu na sehemu ya juu ya tunda. Ulinganifu wa kuenea kwa vidonda kutokea katikati ya mipasuko na kufanya mzunguko unaweza kupelekea matatizo tofauti ya kimaumbile. Wakati mwingine kitako cha tunda pia huathiriwa. Matunda yakiathiriwa ikiwa bado ni machanga, ndivyo mipasuko husababisha uharibifu zaidi. Nyufa na mipasuko pia huweza kutokea kwenye shina. Ugonjwa huu ni kutokana na tunda kukua zaidi na kuzidi uwezo wa kutanuka kwa ngozi yake: Mnyumbuliko wa ngozi huzidiwa na nyufa ndogo huonekana, ambazo hatimaye hupasuka na kuwa wazi.
Hakuna matibabu ya kibaolojia ya ugonjwa huu. Unaweza kutibiwa tu na hatua za kuzuia.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ugonjwa huu unaweza kutibiwa tu kwa kutumia hatua za kuzuia. Hata hivyo, epuka matumizi yaliyo zidi ya mbolea ya naitrojeni na kuwa makini na kiwango cha potasiamu ya udongo.
Nyufa na mipasuko husababishwa na ukuaji wa ghafla na wa haraka wa tunda, kwa kawaida huhusishwa na ufyonzaji mwingi wa maji wa mmea. Mabadiliko haya ya ghafla katika ukuaji wa mmea yanaweza kuchochewa na mabadiliko ya hali ya mazingira kama vile mabadiliko kutoka kipindi cha baridi na mvua, na unyevu mwingi hadi joto na ukavu. Kuweka mbolea kwa uwiano sahihi pia ni muhimu ili kuepuka tatizo. Kwa mfano, matumizi mengi ya naitrojeni na upatikanaji mdogo wa potasiamu wakati wa ukuaji wa maua na matunda utapelekea ukuaji uliozidi wa tunda na kuonekana kwa nyufa.