Nyanya

Ugonjwa wa Uso wa Paka wa Nyanya

Physiological Disorder

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Uharibifu mkubwa, makovu na kupasuka kwa matunda kwenye kitako.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Nyanya

Dalili

Uso wa paka ni kasoro ya kimaumbile inayo sababisha uharibifu na makovu ya matunda, mara nyingi kwenye kitako. Matunda yaliyoathiriwa yana umbo la lenye masikio/matundu kiasi, na makovu ya kahawia kati ya maskio tofauti ambayo yanaweza kuenea kuelekea ndani ya nyama. Haipaswi kuchanganywa na mipasuko mduara au mviringo ya tunda. Ingawa hayawezi kuuzwa, matunda yenye umbo mbovu bado huhifadhi ladha yake na yanaweza kuliwa kwa usalama. Sababu zinazowezekana ni hali ya hewa ya baridi na joto la usiku chini ya 12°C wakati wa maua, viwango vya juu vya naitrojeni, na majeraha yanayo tokana na dawa za kuua magugu. Aina za nyanya zilizo na matunda makubwa sana zina athiriwa zaidi.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Ugonjwa huu unaweza kutibiwa tu kwa hatua za kuzuia.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ugonjwa huu unaweza kutibiwa tu na hatua za kuzuia ambazo ni rahisi kutekeleza. Hata hivyo, epuka matumizi ya viua magugu ambavyo vinaweza kusababisha hali hiyo katika aina zinazo shambuliwa.

Ni nini kilisababisha?

Sababu hasa za sura ya paka kwenye nyanya hazijulikani lakini kwa ujumla hutokea zaidi kwenye aina zenye matunda makubwa. Halijoto ya chini ya usiku (12°C au chini) kwa siku kadhaa mfululizo wakati wa ukuzaji wa vitumba vya maua huambatana na ugonjwa huu wa kimaumbile, pengine kutokana na uchavushaji usiokamilika wa ua. Baadhi ya aina zinaweza kuathiriwa zaidi na mabadiliko haya ya joto. Vikwazo vingine vya ukuaji wa vitumba vya maua pia vinaweza kusababisha kasoro ya uso wa paka. Uharibifu wa kimaumbile wa maua, kupogoa kwa nguvu au kuathiriwa na baadhi ya dawa za kuua magugu (2, 4-D) pia kunaweza kusababisha matunda kuwa na umbo bovu. Ukuaji wa matunda kupita kiasi kwa sababu ya uwekaji mbolea usio sawia wa naitrojeni pia unaweza kuwa sababu. Hatimaye, uharibifu wa vithiripi au hali inayojulikana kama jani dogo la nyanya pia vinahusika kusababisha kasoro ya uso wa paka.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina, ambazo zinastahimili mabadiliko ya joto.
  • Epuka matumizi ya dawa za kuua magugu ambazo zinaweza kusababisha hali hii.
  • Kufuatilia mara kwa mara hali ya joto wakati wa maendeleo ya vitumba vya maua.
  • Epuka majeraha ya mimea wakati wa kazi za shambani.
  • Fuatilia viwango vya naitrojeni kwenye udongo kabla ya kuweka mbolea.

Pakua Plantix