Herbicides Photosynthesis Inhibitors
Nyingine
Majani hutengeneza umanjano au madoa doa kati ya mishipa ya jani, na kusababisha tishu kati ya mishipa kuwa za manjano. Katika hatua za baadaye, kingo za majani zinakuwa za manjano huku mishipa ya jani ikibaki ya kijani. Polepole, majani hukauka na yanaweza kudondoka ndani ya siku mbili hadi tano, yakionekana kama 'mfuko wa karatasi'.
Hakuna suluhisho za kudhibiti uharibifu kwa njia ya kibaolojia. Kinga na mbinu nzuri za kilimo ndizo njia muhimu za kuepuka madhara.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kinga na matibabu ya kibaolojia, ikiwa yanapatikana. Kabla ya kupanga kupulizia dawa ya kuua magugu, hakikisha unajua aina ya magugu unayokabiliana nayo (kimsingi magugu yenye majani mapana dhidi ya nyasi) na chagua mbinu bora zilizopo. Chagua dawa ya kuua magugu kwa uangalifu, kwa kusoma lebo kwa uangalifu na kufuata maelekezo ya dozi kama ilivyoonyeshwa kwenye lebo.
Dalili zinategemea bidhaa za dawa zilizotumika, dozi, na wakati dawa ilipotumiwa. Uharibifu husababishwa na dawa za kuua magugu za kundi C, kama vile atrazine, bromoxynil, diuron, na fluometuron. Kutokana na athari zao zinazotokea kwa haraka na athari za madhara kwenye majani, mara nyingi hujulikana kama 'wapaushaji', yaani dawa zinazopausha majani. Dawa hizi huzuia usanidi mwanga na kuharibu rangi ya kijani iliyomo kwenye seli, na hivyo kubadilisha rangi yake ya asili. Majani ya zamani yanaathiriwa zaidi kuliko majani machanga. Dalili zinatokea kwa haraka zaidi panapo kuwa na mwanga wa jua mkali. Matatizo ya kukua kwa usugu dhidi ya dawa hizi ni jambo la kawaida kwa aina kadhaa za magugu (kwa mfano, nyasi, mharadali, upupu, na figili mwitu).