Pilipili Hoho & Pilipili

Kuungua na Jua

Abiotic Sunburn

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Kunyauka na majani kuwa ya njano, kuanzia pembezoni.
  • Matunda na gome pia huathirika baada ya kupukutika kwa majani.

Inaweza pia kupatikana kwenye

59 Mazao
Mlozi
Tufaha
Aprikoti
Ndizi
Zaidi

Pilipili Hoho & Pilipili

Dalili

Kuungua na jua kusiko kwa asili humaanisha uharibifu unaosababishwa kwa mimea, vichaka au miti kwa mjumuiko wa mionzi ya jua ya moja kwa moja na joto kupita kiasi. Sababu hizi hubadilisha unyevu kwenye tishu za mmea, na kusababisha mwanzo wa kunyauka kwa majani machanga, laini. Majani haya polepole yanageuka kijani mpauko na huanza kupata vidonda karibu na ncha na kingo baada ya siku 2-3. Vidonda vilivyo kauka baadaye huendelea kuelekea katikati ya uso wa jani. Upukutishaji wa majani unaosababishwa na mfadhaiko wa ukame au mashambulizi ya wadudu pia yanaweza kusababisha jua kubabua matunda au gome, kwa kuwa hayana kivuli na majani tena. Kwenye gome inaweza kuchukua muundo wa nyufa na vikwachu/vidonda gome ambayo hatimaye huendelea na kuwa kama sehemu zilizo kufa kwenye shina.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Udongo mweupe wa mfinyanzi au michanganyiko ya ulanga inaweza kunyunyiziwa kwenye majani na shina ili kuzuia mwanga wa jua. Hii inaweza kupunguza joto kwa 5-10 ° C. Bidhaa zinazotokana na calcium carbonate au chokaa ya fuwele pia zinapendekezwa. Bidhaa za nta ya Carnauba hutumika kama kinga ya asili kwa mimea.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Tindikali ya abscisic ikitumika kama mbolea ya ziada husaidia kupunguza madhara ya kuchomwa na jua kwa matunda kama vile tufaha na hivyo inaweza kufanya kazi katika mazao mengine. Bidhaa za kuzuia upotevu wa maji kupitia majani, kama vile zile za poly-1-P menthene, pia zimeonyesha matokeo mazuri katika baadhi ya tafiti.

Ni nini kilisababisha?

Majeraha ya kuchomwa na jua ni jambo la kawaida katika mimea au miti inayokuzwa katika maeneo yenye mionzi mikali ya jua, joto la juu la hewa na kiasi cha chini cha unyevu. Mwinuko pia huchangia kwani mionzi ya urujuani (UV) ni mikubwa zaidi kwenye miinuko ya juu. Dalili huonekana kwenye majani, matunda na gome. Matukio na ukali wa kuungua na jua hutegemea mambo kama vile aina mbalimbali za mmea, hatua ya ukuaji wake na unyevu wa udongo. Kuungua na jua ni kwa hali ya juu hasa wakati joto la hewa na idadi ya masaa ya jua ni kubwa wakati wa kukomaa/kuiva. Mbadilishano wa matukio ya hali ya hewa pia ni muhimu: kwa hivyo, uharibifu unaweza pia kutokea wakati hali ya hewa ya baridi au tulivu inafuatwa ghafla na hali ya hewa ya joto na ya jua.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia aina zinazostahimili kuungua na jua.
  • Hakikisha kwamba umwagiliaji unaendana vyema na mahitaji ya maji ya zao hilo.
  • Mwagilia maji kabla ya mawimbi ya joto ili kuepuka matatizo ya mimea na kuchomwa na jua.
  • Epuka kupogoa kupita kiasi majira ya joto na kukata majani.
  • Boresha mzunguko wa hewa kupitia dari/kivuli.
  • Weka mfumo wa kinyunyizio cha kupoza mimea au miti.
  • Vyandarua/neti za kivuli au mifuko ya matunda pia inaweza kuwekwa ikihitajika.
  • Tumia mazao ya kivuli kati ya mistari ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji kwenye udongo (kwa mfano, mahindi au mbaazi kwenye shamba la mananasi).

Pakua Plantix