Adventitious roots
Nyingine
Vitu kama matuta, vifundo vidogo, uvimbe, au vinyweleo vidogo kwenye mashina ya mimea. Vinaweza kuonekana katika sehemu tofauti kwenye shina.
Hakuna udhibiti wa kibayolojia unaohitajika kwa suala hili lisilo na madhara; fuata tu hatua za kuzuia ili kuepusha tatizo hilo.
Hakuna udhibiti wa kemikali unaohitajika kwa suala hili lisilo na madhara; fuata tu hatua za kuzuia ili kuepusha tatizo hilo.
Vijiuvimbe hivyo havina madhara, hata hivyo vinaweza kuwa ishara kwamba mmea wa nyanya unafadhaika. Mfadhaiko huo unaweza kutokana na uharibifu kwenye mfumo wa mizizi, umwagiliaji mbaya, unyevu wa juu, au maambukizi ya kuvu. Mizizi hii ni mwitikio wa asili wa mmea kumudu na kukabiliana na visababishi vya mfadhaiko huo. Pia ifahamike kuwa aina fulani za nyanya zilizowekwa chini ya hali fulani za uzalishaji (unyevu kupita kiasi, ukosefu wa maji) zinaweza kuzalisha mizizi ya ziada kwenye shina ili kukabiliana na hali hizo. Aina za kienyeji zinakabiliwa zaidi na kuota kwa mizizi ya ziada kwenye shina.