Blossom drop
Nyingine
Mimea huchanua, lakini maua mara nyingi hufa na kuanguka. Wakati mwingine, kabla ya kuanguka, vikonyo vya maua hugeuka na kuwa vya njano.
Udhibiti wa asili unahusisha hasa kuchukua hatua za kuzuia. Hakikisha umeangalia ikiwa vidhibiti ukuaji wa mimea vinaruhusiwa kwa bidhaa zako za asili. Ikiwa ndivyo, soma miongozo ya udhibiti wa kikemikali.
Wakulima wanaweza kulinda maua zaidi kwenye mimea yao ya kwenye vitalu nyumba kwa kutumia dawa maalum kama vile GA3 au NAA. Ni muhimu kunyunyiza maua kwa wakati unaofaa, kama vile maagizo yanavyosema. Kumbuka kwamba dawa hizi zinaweza zisifanye kazi kila wakati kwa sababu vitu vingi tofauti vinaweza kuathiri utokaji wa maua. Hii sio suluhisho kwa kila tatizo.
Kuanguka kwa maua kunaweza kusababishwa na sababu ambazo zinavuruga uchavushaji maua na afya ya mmea au kutokuwepo kwa wadudu wachavushaji. Joto la chini na la juu, pamoja na viwango vya chini na vya juu vya unyevu ambavyo havifai baada ya maua kuchavuliwa, ni sababu muhimu. Naitrojeni nyingi huchochea majani kukua badala ya maua, na hivyo kusababisha ukuaji duni wa matunda, wakati naitrojeni kidogo husababisha mimea dhaifu ambayo haiwezi kuhimili matunda. Ukosefu wa maji ya kutosha hudhoofisha mimea, na maji mengi kupita kiasi yanaweza kuikosesha mizizi hewa na kusababisha maua kuanguka. Vithiripi na utitiri huharibu tishu za mmea na kusababisha maua kuanguka, na magonjwa ya ukungu/kuvu hudhoofisha mimea hivyo pia hupelekea maua kuanguka/kupukutika.