Nyanya

Majeraha ya Dawa ya Kuua Magugu

Herbicide Shikimic acid pathway inhibitors

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Kuonekana kwa majani yaliyodumaa, manjano na hatimaye majani yenye tishu zilizokufa.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Nyanya

Dalili

Dalili za mwanzo huonyesha kubadilika rangi nyeupe/njano chini ya majani machanga. Majani/vipande vya majani huonekana vidogo na vime kunjwakunjwa na kingo za kahawia na vimefungwa juu. Maua machache yanazalishwa na kusababisha hasara ya mavuno. Matunda yana ulemavu na ni madogo na makovu ya hudhurungi iliyokolea. Katika hali mbaya, kufa kwa tishu kawaida huanza juu ya mmea na kuelekea chini.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna

Udhibiti wa Kemikali

Hakuna

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na matumizi yasiyofaa ya dawa ya wigo mpana ya glyphosate. Hii husababishwa na kupeperushwa kwa dawa ama kutokana na matumizi ya mkulima mwenyewe, jirani au kutoka kwa mabaki ya glyphosate kwenye kinyunyizio cha matumizi tofauti ya dawa na inaweza kuathiri spishi za mimea isiyolengwa. Dawa ya kuua magugu huwekwa kwenye majani na husafirishwa katika mmea wote. Inaua mimea kwa kuingilia kemikali ya mmea ambayo ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji wa amino asidi zinazohitajika kwa ukuaji mpya. Uambukizaji unaweza pia kutokea kupitia uchafuzi usiolengwa kama vile kupeperuka, uchafuzi wa kinyunyizio, kubeba kwenye udongo, ufukivu, matumizi ya bahati mbaya n.k. Kiwango cha uharibifu hutegemea mambo kama vile kiasi cha mfiduo, hali ya kukua, aina zilizoathirika na hatua ya ukuaji. Uharibifu unaweza kuwa mkubwa na mara nyingi husababisha hasara ya kudumu ya mimea yenye thamani.


Hatua za Kuzuia

  • Mwagilia na weka mbolea mimea ili kukuza afya njema.
  • Soma na ufuate maagizo ya lebo kwenye kemikali zote, pamoja na matumizi ya mbolea iliyopendekezwa kwa viwango vinavyofaa.
  • Rekebisha kinyunyizio na kuwa mwangalifu unapoweka dawa ya kuua magugu karibu na mimea.
  • Epuka kunyunyiza wakati wa hali ya hewa ya baridi na ya mvua kwani dawa hufanya kazi polepole katika kipindi hiki.
  • Weka dawa za kuua magugu wakati kasi ya upepo iko chini na mwelekeo wake ni wa kiwango cha chini sana cha kupeperusha.
  • Epuka kutumia vifaa vya kupulizia viua magugu kuwekea dawa za kuua wadudu au kuvu.
  • Kwa kawaida, ni vigumu kuzuia jeraha mara tu dalili zinapoonekana.
  • Hata hivyo, ikiwa dalili si kali na mmea haufi, ukuaji mpya unaweza kuwa ni kawaida kutokea.

Pakua Plantix