Rapid Growth Syndrome
Nyingine
Kutokea kwa mchapuko mkali katika kasi ya ukuaji wa mmea. Majani ya mahindi hushindwa kukunjuka vizuri, na majani yaliyojiviringisha yanakuwa yamefungashwa pamoja kwa nguvu. Majani mapya yanayokua haraka hushindwa kujitokeza na husababisha majani yaliyojiviringisha kupinda na kujisokota wakati yanapojaribu kuchomoza. Majani yaliyokwama kwenye mviringisho mara nyingi huwa na rangi ya manjano angavu pale yanapojitokeza, na hivyo kuwa rahisi kuyaona shambani. Majani yaliyoathirika yanaweza kuwa na mikunjo mithili ya makunyanzi karibu na kitako cha shina na yatabaki hivyo katika msimu mzima wa ukuaji.
Kama ilivyo kwa athari nyingi zinazohusiana na msongo wa hali ya hewa, ni kawaida kwa baadhi ya mazao/mbegu chotara kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata tatizo hili kuliko mazao yasiyo chotara. Chagua aina ya mbegu au aina ya mazao chotara yanayofaa kwa eneo lako.
Udhibiti wa kemikali hauna umuhimu kwenye tatizo hili.
Uharibifu huu kwa kawaida unahusiana na mabadiliko ya ghafla kutoka kwenye hali ya baridi hadi joto, na hivyo kusababisha mchapuko mkali katika kasi ya ukuaji wa mimea. Majani mapya yanayokua kwa haraka hushindwa kuchomoza, na yatasababisha majani yaliyojiviringisha pamoja kupinda na kujisokota pale yanapojaribu kuchomoza. Tatizo hili kwa kawaida hutokea kati ya hatua ya 5 hadi ya 6 ya ukuaji wa mimea, lakini linaweza pia kuonekana hadi hatua ya 12 ya ukuaji wa mimea. Kwa kawaida, hakuna athari kubwa kwa mavuno. Kumbuka kuwa kujisokota kwa majani kunaweza pia kusababishwa na mambo mengine, hususani majeraha yanayosababishwa na dawa za kuua magugu.