Cell injury
Nyingine
Madoa yaliyoungua yenye rangi ya hudhurungi (kahawia) huonekana kati ya mishipa ya majani. Zaidi ya hayo, maua yaliyo chanua na matunda machanga huharibika. Majani huwa na vidonda au shimo kwenye nyuso, pamoja na kubadilika rangi, tishu zilizojaa maji. Tishu zilizojeruhiwa huonekana kuwa utomvu na zinaweza kutoa harufu mbaya. Majani yanaweza kuanguka mapema.
Kwa vile ni jambo la asili udhibiti wa kibayolojia hauwezekani.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Kwa kuwa ni tukio la asili udhibiti wa kemikali hauwezekani.
Uharibifu wa theluji hutokea wakati barafu imejiunda ndani ya tishu za mmea na kuumiza seli za mmea, kwa hiyo ni kutengenezeka kwa barafu ndiko huumiza mmea na sio hali ya baridi. Upepo wa baridi huondoa unyevu kutoka kwenye majani ya kijani kibichi zaidi kuliko ambavyo hutokea kwenye mizizi. Hii husababisha rangi ya majani kuwa kahawia hasa kwenye ncha na ukingo wa majani. Mimea michanga huathirika zaidi na uharibifu wa theluji kuliko mimea ambayo imesha imarika kikamilifu.