Chimera
Nyingine
Rangirangi za majani hujionyesha kwa mabadiliko ya rangi yasiyo sawa kutoka rangi nyeupe hadi za njano kwenye sehemu za majani au wakati mwingine mashina. Tishu zenye rangi ya kijani ya kawaida zipo jirani, na hivyo kusababisha muundo wa nakshi ya kipekee, viraka au mistari. Wakati mwingine rangirangi ya mishipa hutokea, ambapo mishipa ya majani hubadilika rangi huku sehemu nyingine za tishu za jani zikibaki na rangi ya kijani kibichi. Ikiwa sehemu kubwa za mmea zinaathiriwa, ukosefu wa umbijani unaweza kusababisha ukuaji uliodumaa. Hata hivyo, mara nyingi upungufu huu huathiri asilimia ndogo tu ya shamba na haiathiri mavuno.
Kwa kuwa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kimazingira inayosababisha tatizo hili, hakuna tiba za kibaolojia kwa ajili ya kutibu hali hii.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaolojia ikiwa zinapatikana. Rangirangi ya majani ni tatizo la kijenetiki au kimaumbilei na kwa hivyo hakuna bidhaa za kemikali zinazotibu hali hii.
Rangi rangi ya majani inatokana na kasoro ya kijenetiki/kinasaba au kimaumbile ambayo haihusiani na hali za kimazingira, yaani, hakuna vimelea vinavyohusika. Sababu kuu ya rangirangi za majani ni ukosefu wa rangi asili umbijani kwenye baadhi ya sehemu za tishu za majani. Hutokea kwa kiwango kidogo kiasili na sio tishio kwa mimea au mavuno. Hata hivyo, baadhi ya mimea ya mapambo na mimea ya bustani kiasili huwa na rangi rangi, na ni sehemu ya urembo wake.