Nyanya

Ugonjwa wa Kujikunja kwa Majani wa Nyanya

Physiological Disorder

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Majani kuharibika umbo na kubadilika rangi.
  • Majani kukakamaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Nyanya

Dalili

Kama jina linavyo jieleza, dalili zinaweza kuoneshwa na uharibifu wa umbo la majani. Kujikunja kwa awali huanzia kwenye majani ya chini na kuendelea juu ikifuatiwa na mkunjo wa kuelekea ndani kwa urefu. Kawaida, hupona ikiwa hali ya mazingira na sababu za kitamaduni zitarekebika ili kupunguza mfadhaiko. Majani yanaweza kuonekana meupe, yame dumaa, na kingo za njano au mishipa ya zambarau upande wa chini.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Hakuna matibabu ya kibaolojia yanayojulikana dhidi ya ugonjwa huu wa kimaumbile. Unaweza kutibiwa tu kwa hatua za kuzuia.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibayolojia, ikiwa yanapatikana. Ugonjwa huu wa kimaumbile unaweza kutibiwa tu na hatua za kuzuia.

Ni nini kilisababisha?

Kasoro ya kimaumbile ya kujikunja majani hutokea kutokana na matatizo ya kimazingira. Unyevu mwingi na viwango vya juu vya naitrojeni ndio sababu kuu za kuharibika kwa umbo la majani, pamoja na joto, hali kavu, kupogoa sana, uharibifu wa mizizi, na mshtuko wa kupandikiza. Dalili za kujikunja kwa majani pia hupatikana na zinaweza kufanana na maambukizi ya virusi. Kwa mfano, inzi weupe husambaza virusi (Yellow Leaf Curl Virus - YLCV) ambayo husababisha majani mapya kuwa na umbo la kikombe.


Hatua za Kuzuia

  • Panda aina maalum za mimea kwenye udongo usiotuamisha maji.
  • Dudumisha unyevu wa kutosha na sawia kwenye udongo.
  • Epuka matumizi makubwa ya mbolea, hasa za naitrojeni.
  • Weka fosforasi kwa kiwango sahihi.
  • Epuka upogoaji mkali na udumishe halijoto chini ya 35°C kwa kuweka kivuli au kupoza kwa kuvukiza.

Pakua Plantix