Physiological Disorder
Nyingine
Ugonjwa wa zipu ni kasoro ya kimaumbile inayosababisha makovu membamba ya rangi ya kahawia ambayo hupita kando ya tunda, na hatimaye kusababisha mipasuko ya sehemu husika. Makovu huenea kiasi kando ya matunda kwenye urefu na upana wake, mara chache huunganisha kitako cha tunda na kikonyo kwa muundo wa kidonda kinachofanana na zipu, ndiyo chanzo cha jina. Vifuo ndani ya nyama ya matunda na kuharibika kwa uso wa tunda pia ni vya kawaida. Tishu zilizoharibiwa hupoteza unyumbulifu wake na matunda hayakui vizuri. Mara uharibifu unapoonekana, tayari itakua umechelewa sana kufanya chochote.
Hakuna matibabu ya kibaolojia yanayojulikana dhidi ya kasoro hii ya kimaumbile. Inaweza kutibiwa tu na hatua za kuzuia.
Daima zingatia mbinu jumuishi yenye hatua za kinga na matibabu ya kibayolojia ikiwa yanapatikana. Ugonjwa huu unaweza kutibiwa tu kwa hatua za kuzuia.
Ugonjwa wa zipu ni kasoro ya kimaumbile, inayosababishwa na joto la chini na unyevu wa juu mwishoni mwa uwekaji wa maua na mwanzoni mwa uwekaji matunda. Wakati wa kutokea kwa matunda machanga, mbelewele moja au kadhaa hubakia kwenye ukuta wa ovari, na kusababisha makovu lainik nje ya ngozi ya matunda kadri yanavyo endelea. Unyeti wa joto hutofautiana kutoka kwa aina hadi aina. Baadhi ya aina za nyanya zinakabiliwa zaidi kuliko nyingine, huku nyanya za Beefsteak zikiwa miongoni mwa zinazo athirika zaidi.