Schizotetranychus hindustanicus
Mchwa
Uharibifu hujulikana kwa kuonekana kwa madoa madogo ya rangi ya kijivu au fedha kwenye upande wa juu wa majani, mchakato unaoitwa utokeaji wa madoa. Madoa haya mara nyingi huwa mengi zaidi kando ya vena kuu (mshipa wa katikati wa jani) na baadaye yanaenea kwenye jani lote. Kwa kawaida, majani, matunda, na matawi yaliyo pembezoni mwa mti ndio huwa kwenye uwezekano wa kushambuliwa zaidi. Katika viwango vya juu vya maambukizi, madoa haya huungana na kuwa madoa makubwa na kuyafanya majani au matunda ya kijani/mabichi kuwa na muonekano wa rangi ya fedha au shaba nyeusi. Tishu zilizoshambuliwa polepole zinakuwa ngumu na kuoza, na kusababisha kuanguka mapema kwa majani, kufa kwa matawi, kupungua kwa ubora wa matunda, na kupungua kwa uimara wa miti. Hali hii hutokea zaidi hususani wakati wa hali mbaya ya kimazingira, kama vile hali ya hewa kavu na yenye upepo. Kinyume chake, ugavi mzuri wa maji hupunguza matukio ya wadudu na uharibifu unaosababishwa na wadudu hawa.
Utitiri hawa wana idadi kubwa ya wadudu wanaowawinda na kula wadudu wengine na pia maadui wa asili, ambao mara nyingi hutosha kudhibiti kuenea kwao ikiwa hali ya hewa si nzuri kwa wadudu hawa. Kwa sababu ya viota vya utando, utitiri aina ya phytoseiid (kwa mfano, Euseius stipulatus) hawana ufanisi dhidi ya utitiri wa Kihindu. Baadhi ya aina za wadudu-kibibi (ladybird) wa jenasi ya Stethorus huwala utitiri wa Kihindu kwa uroho mkubwa. Kuvu, na hususani virusi, pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kudhibiti idadi ya utitiri shambani, jambo ambalo linaweza kuchochewa na joto.
Daima zingatia mbinu jumuishi zinazotumia hatua za kuzuia pamoja na matibabu ya kibaolojia ikiwa yanavyopatikana. Dawa za kuua wadudu zinazoweza kuchagua wadudu waharibifu pekee ndizo zinapendekezwa zaidi, kwa sababu dawa zinazoua wadudu wa aina mbalimbali, zinaweza kuongeza tatizo kwa kuua wadudu wawindaji na wadudu wengine wenye manufaa. Utumiaji wa madawa ya acaricides kwa mzunguko huzuia kutokea kwa usugu wa utitiri dhidi ya madawa.
Dalili husababishwa na utitiri kamili na tunutu wa utitiri wa Kihindu wa mimea jamii ya michu ngwa, kwa jina la kisayansi akifahamika kama Schizotetranychus hindustanicus. Utitiri hawa hufahamika kwa viota vya utando wa kipekee (1-3 mm kwa kipenyo) ambavyo majike huvitengeneza upande wa chini wa majani na kukaliwa na kundi la utitiri. Sifa hii inawatofautisha na utitiri wengine na hivyo kupata jina lao lingine maarufu la 'utitiri-watengeneza viota-vya utando'. Utitiri wakubwa/waliokomaa hutoka kwenye kiota na kushambulia majani mengine au tishu za matunda, wakati utitiri ambao hawajakomaa hupendelea kukaa ndani ya utando. Wadudu na ndege wanaweza kusambaza utitiri kwenye miti mingine. Zana za kilimo zilizoambukizwa na kanuni mbaya za shamba zinaweza pia kusambaza wadudu waharibifu kwenye mashamba mengine. Mpango mzuri wa umwagiliaji wenye ugavi bora wa maji kwa ajili ya miti hupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya uwepo wa wadudu waharibifu na uharibifu unaosababishwa na wadudu hawa. Kinyume chake, unyevu wa chini au wa juu, upepo mkali, ukame, au mfumo dhaifu wa ukuaji wa mizizi unaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi.