Sugar Spot
Nyingine
Dalili zitaonekana baada ya ndizi kuvunwa. Mwanzoni, madoa madogo meusi hujitokeza kwenye ganda la ndizi, ambayo yanaweza kuongezeka kadri muda unavyoenda. Madoa ya kahawia pia yanaweza kuonekana kwenye nyama ya tunda.
Hakuna matibabu ya kibiolojia yanayohitajika au yanayopatikana, kwani mchakato wa ukuaji wa tunda ni wa asili.
Hakuna matibabu ya kemikali yanayohitajika au yanayopatikana, kwa sababu mchakato wa ukuaji wa tunda ni wa asili.
Dalili hizi husababishwa na mchakato wa kawaida wa kuiva kwa ndizi. Ndizi huendelea kuiva hata baada ya kuvunwa. Madoa hayo huashiria kuwa wanga unabadilishwa kuwa sukari, kumaanisha kwamba idadi kubwa ya madoa ya kahawia inaonyesha kiwango kikubwa cha sukari. Kimeng'enya (enzemu) kinachoitwa polyphenol oxidase au tyrosinase kinapokutana na oksijeni inaaminika kusababisha madoa ya kahawia. Homoni za ethilini hukutana na tindikali (asidi) za tunda na kuzivunja, na hivyo kusababisha ulainikaji wa ndizi. Mchakato wa kawaida wa kuwa na rangi ya kahawia na kulainika huwa dhahiri wakati tunda linapokuwa na michubuko.