Oxya intricata & Locusta migratoria manilensis
Mdudu
Dalili hutofautiana kutegemea na aina ya mmea na njaa ya panzi. Panzi na nzige wanakula hasa majani, wakiharibu kingo au kukata sehemu kubwa za jani. Nafaka, vitumba vya mbegu, na matunda pia vinaweza kushambuliwa na mdudu huyu. Wanapokuwa na njaa sana, wanaweza kula hata mashina na magome. Pia hula vishina, na hivyo hukata sehemu za uzazi za mmea.
Viumbe hai wa udhibiti wa kibaolojia wanaopatikana kwa njia asilia kama vile nyuki, vimelea wa nzi na minyoo, wadudu jamii ya mchwa (mchwa, majimoto, siafu, nyenyere, n.k), ndege, chura, na buibui wanaotandika utando, wote hao ni muhimu katika kudhibiti panzi na nzige kibaiolojia. Vimelea vya magonjwa ya kuvu/ukungu na kuvu kiuawadudu (yaani kuvu, wanaoshambulia wadudu) pia wanaweza kutumika kupunguza idadi ya tunutu (panzi wachanga). Tumia mtego ya chambo yenye sumu iliyoandaliwa nyumbani kwa kutumia maji ya chumvi na makapi ya mpunga.
Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Tumia dawa za kuua wadudu za kupulizia kwenye majani ili kudhibiti panzi katika mashamba yanayoonyesha uharibifu wa zaidi ya asilimia 10. Dawa za chembe chembe za ungaunga hazifai. Mitego ya chambo zenye sumu inaweza kutumika kuwavutia panzi wakubwa. Dawa za kuua wadudu zinazoweza kupuliziwa dhidi ya mdudu huyu ni pamoja na chlorpyriphos, buprofezin au etofenprox. Dawa zingine zinazopendekezwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, yaani FAO ni pamoja na bandiocarb 80% WP ambayo kiwango cha matumizi ni gramu125 kwa kila hekta moja, chlorpyriphos 50% EC kwa kiwango cha mililita 480 kwa hekta moja, na deltamethrin 2.8% EC kwa kiwango cha mili lita 450 kwa hekta. Zingatia kwamba, hekta moja ni sawa na ekari mbili na nusu.
Dalili za kipekee kwenye majani na masuke husababishwa na tunutu(panzi wachanga) na panzi kamili (waliopevuka). Mazingira ya kwenye maji ni muafaka kwa ukuaji wao (kwa mfano, mashamba ya mpunga, maeneo yenye mafuriko, na kwenye delta). Panzi wanakuwa na urefu wa kuanzia milimita 5 hadi sentimita 11, na wanaweza kuwa ama warefu na wembamba au wafupi na wanene. Wanaweza kujichanganya vizuri katika mazingira yao kwa sababu wanaweza kuwa na rangi ya kijani au rangi ya majani makavu. Majike hutaga mayai ya rangi ya njano kwenye majani. Panzi kamili (wakubwa) wanaweza kuwa na mbawa, kuwa katika makundi, na kuhama.