Zabibu

Ubwiri Unyoya wa Zabibu

Plasmopara viticola

Kuvu

Kwa Ufupi

  • Kwenye majani kuna madoa yenye hali ya mafuta na rangi ya kijani-manjano yakiwa na mduara angavu.
  • Madoa hubadilika na kuwa mabaka ya kahawia yasiyo na umbo maalum.
  • Utando mweupe hadi kijivu ulio mithili ya pamba chini ya madoa.
  • Ugonjwa unaweza kuathiri machipukizi, vitawi, na maua.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

1 Mazao

Zabibu

Dalili

Katika majani machanga, madoa ya kijani-manjano yenye hali ya mafuta, mara nyingi yakiwa yamezungukwa na mduara angavu wenye rangi ya kahawia, yanaonekana upande wa juu. Kadri ugonjwa unavyoendelea, madoa yanaongezeka ukubwa na katikati ya maeneo yaliyoathirika yanakauka, yakitengeneza mabaka yasiyo na umbo maalumu yenye rangi mbalimbali za kahawia. Baada ya mfululizo wa usiku wa joto na unyevunyevu, utando mzito mithili ya pamba wenye rangi nyeupe hadi kijivu hutokea chini ya madoa. Ikiwa maambukizi yanatokea kwenye majani yaliyo komaa baadaye katika msimu, basi dalili hutambulika kwa majani kubadilika rangi kati ya mishipa na kuwa ya manjano; rangi ambayo polepole inaunda nakshi ya mozaiki ya kahawia. Maeneo ya kahawia yenye hali ya mafuta na ukuaji wa kuvu/ukungu pia unaweza kuonekana kwenye machipukizi, vitawi na maua. Kuanguka kwa majani na kufa au kudumaa kwa machipukizi machanga na maua kunasababisha kudumaa kwa ukuaji wa mmea na mavuno duni.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Dawa za asili za kudhibiti kuvu zinazotumika kabla ya maambukizi kwenye mimea ni pamoja na dawa zinazotokana na na shaba, kama vile mchanganyiko wa Bordeaux.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kukinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia ikiwa yanapatikana. Dawa za kukinga mazao dhidi ya kuvu/ukungu zinaweza kusaidia kuzuia kuathiriwa kwa mimea lakini zinapaswa kupulizwa vizuri kwenye upande wa chini wa majani. Dawa za kuua/kukinga kuvu zinazotokana na shaba, kama vile mchanganyiko wa Bordeaux na dithiocarbamates zinaweza kutumika. Dawa za kuua kuvu baada ya maambukizi zinapaswa kutumika mara moja baada ya kugundua dalili za kwanza. Dawa za kuua kuvu ambazo kwa kawaida hutumika ya baada ya maambukizi ni pamoja na fosetyl-aluminum na phenylamides.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizo zinasababishwa na kuvu/fangasi anayeitwa Plasmopara viticola na anajulikana kuwa na madhara makubwa katika maeneo ya uzalishaji wa divai yenye mvua za mara kwa mara wakati wa majira ya kuchipua na na ya joto; pamoja na joto juu ya 10°C. Kuvu hawa wanaishi msimu wote wa baridi kwenye mabaki ya mimea iliyoathiriwa katika udongo au kwenye machipukizi yenye ugonjwa. Upepo na rasharasha za mvua husambaza vijimbegu (kwa jina lingine viiniyoga) vya kuvu wakati wa majira ya mvua. Vijimbegu vya kuvu huota na kutengeneza umbile ambalo huingia kwenye jani kupitia vishimo vilivyo upande wa chini wa majani. Kutokea hapo vijimbegu vya kuvu vinaanza kuenea kupitia tishu, hatimae kuzizidi tishu za ndani na kutengeneza utando wa ukungu kwa nje. Kuvu inaweza kukua katika hali ya joto kati ya 13 na 30°C. Ukuaji bora hufanyika kati ya nyuzi joto 18 hadi 25°C, ikifuatia mfululizo wa usiku wa joto na unyevunyevu.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha udongo unapitisha maji vizuri.
  • Chagua aina za mbegu zenye ukinzani dhidi ya magonjwa kama zinapatikana.
  • Panda katika maeneo yanayopata mwanga wa jua vizuri na chagua mwelekeo sahihi.
  • Hakikisha kuna nafasi ya kutosha kati ya mzabibu na mzabibu na pia kuna uingizaji mzuri wa hewa.
  • Inua mizabibu kutoka ardhini na ifunge vizuri.
  • Dhibiti magugu ndani na karibu na shamba.
  • Ondoa mabaki ya mimea kutoka shambani.
  • Weka zana na vifaa vyako vya kilimo vikiwa safi.
  • Epuka kusambaza udongo na mimea iliyoathiriwa.
  • Hakikisha unatumia mbolea kwa viwango vyenye uwiano ili kuimarisha mimea.

Pakua Plantix