Idioscopus spp.
Mdudu
Tunutu na wadudu kamili wa spishi za Vijasidi (Mruka jani) hufyonza utomvu wa floemu kutoka kwenye vitawi, maua, majani laini, na matunda. Tishu za mimea zilizoathiriwa hugeuka kahawia, na zinaweza kubadilika umbo na kukauka. Maua machanga hushindwa kukua, hivyo kuathiri utungaji na ukuaji wa matunda. Wakati wanapokula kwenye miembe, vijasidi (waruka-jani) huzalisha majimaji yenye sukari (umande wa asali) ambao huvutia wadudu wengine na kutengeneza mazingira bora kwa ukuaji wa kuvu(ukungu) ulio mithili ya masizi. Ukuaji wa kuvu(ukungu) kwenye majani huathiri usanisinuru, hivyo kuathiri uimara wa mti na kupunguza tija yake. Vijasidi (Viruka-jani) wa miembe hutaga mayai yao kwenye majani na mashina ya maua ya miti ya miembe, ambayo pia yanaweza kusababisha uharibifu wa tishu. Vijasidi wa miembe wanaweza kuwa wadudu hatari, na kusababisha upotevu wa mazao hadi asilimia 50.
Wadudu wa kudhibiti kibaolojia kama vile wadudu wanaowinda jamii ya mbawakimia kijani pamoja na mdudu mfyonza mayai jamii ya nyigu (Polynema sp.) wanaweza kupunguza idadi ya vijasidi. Kinyume na hapo, miti ya miembe iliyoathirika inaweza kutibiwa kwa dawa za kupulizia zinazotokana na mafuta zenye kuvu aina ya Beauveria bassiana au Metarhizium anisopliae ambao kiasili kwenye udongo. Inashauriwa matibabu yafanyike kwa kiwango cha mara 2-3 kwa wiki. Dawa za kupulizia zenye mafuta ya mwarobaini (3%) zinaweza pia kupunguza idadi ya vijasidi kwa hadi asilimia 60.
Daima zingatia mbinu jumuishi zinazotumia hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaolojia ikiwa yanapatikana. Tumia dawa za kupulizia zenye cypermethrin (0.4%), kwani dawa hizi zimethibitika kuwa na ufanisi mkubwa. Dawa za wadudu zenye dimethoate zinaweza kudungwa kwenye shina kuu la mti. Inashauriwa kupulizia mara mbili, kwa kuachanisha siku 7, kabla ya kuanza kwa utokaji wa maua, ili kupunguza athari kwa wachavushaji.
Vijasidi (viruka jani) wa miembe kwa kawaida huwa na umbo la kabari, kichwa kipana na cha mviringo, pamoja na macho yenye umbo la tufe. Wadudu kamili wana rangi ya dhahabu au kahawia yenye giza na urefu wa takriban milimeta 4-5. Tunutu (vijasidi wadogo) wana rangi ya kahawia ya manjano, na macho mekundu. Vijasidi wa miembe hutaga mayai yao moja moja kwenye maua madogo, vishipa jani (mishipa ya majani), na lamina (sehemu bapa) ya majani, kutegemea na spishi. Kati ya mayai 100 hadi 200 yanaweza kutagwa. Wanapendelea mazingira yenye kivuli na unyevunyevu wa kiwango cha juu. Vijasidi ( Viruka jani) kamili ni warukaji wazuri na husambaa kwa haraka katika umbali mfupi. Usafirishaji wa miche unaweza kueneza wadudu hawa kwenye bustani au maeneo mengine. Bustani za zamani, zisizotunzwa au zilizopandwa karibu karibu hutengeneza mazingira bora ya kuzaliana kwa wadudu.