Mti wa jamii ya mchungwa

Doa-Jani la Mwani

Cephaleuros virescens

Nyingine

Kwa Ufupi

  • Madoa yenye manyoya, ya kijani hadi ya machungwa kwenye majani.
  • Mipasuko kwenye magome ya mashina machanga.
  • Udondokaji wa majani.
  • Kuharibika kwa umbo la matunda.
  • Kuongezeka kwa maambukizi kwenye matawi yanayoning'inia chini.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Mti wa jamii ya mchungwa

Dalili

Vijidudu vya Ugonjwa wa Doa-jani la Mwani huathiri hasa majani ya maembe na mimea mingine, lakini pia vinaweza kulenga matawi na mashina. Majani yaliyoambukizwa huonyesha madoa ya mviringo, yenye rangi ya kijani hadi machungwa, yaliyoinuka kidogo na yakiwa na kipenyo cha kati ya milimita 2-4. Madoa haya yanatambulika kutokana na ukuaji/utokeaji wa manyoya (Vijimbegu/vijimbegu vya kuvu) na kingo zisizoonekana wazi. Madoa haya yanaweza kuungana na kuwa maeneo yenye mabaka. Katika mashina machanga, ambayo huwa na uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na vimelea vya magonjwa, Ugonjwa wa Doa-jani unaweza kusababisha nyufa kwenye gome, na hivyo kusababisha kufa kwa tawi. Kwa miti mingi, majani ya matawi yanayoning'inia chini huonyesha dalili mbaya zaidi. Ugonjwa wa Doa-jani la Mwani hutokea mara nyingi katika maeneo yenye joto kali na mvua nyingi, na kwenye mimea yenye ukuaji uliodhoofika.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Ikiwa ugonjwa ni mdogo, ondoa na haribu majani yenye madoa pamoja na matawi yaliyoathirika na ugonjwa. Zaidi ya hayo, kusanya na haribu majani yaliyoathirika yaliyoanguka chini. Endapo ugonjwa wa doa-jani la mwani ni mkubwa, pulizia mchanganyiko wa Bordeaux au dawa zingine zinazotokana na shaba. Upuliziaji wa dawa hizi unapaswa kufanyika kila baada ya wiki 2 kuanzia mwanzoni mwa msimu wa joto hadi mwisho wa msimu wa vuli.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye kutumia hatua za kuzuia pamoja na tiba za kibaiolojia ikiwa zinapatikana. Pulizia dawa za kuua kuvu zenye shaba ikiwa udhibiti wa kemikali ni muhimu.

Ni nini kilisababisha?

Ugonjwa wa Doa-jani la Mwani kwa kawaida huonekana katika maeneo yenye joto kali na mvua nyingi, na ambako mimea mbadala inayohifadhi vimelea huwa haikui vizuri. Lishe duni, uwezo duni wa udongo kupitisha maji, na kivuli kikubwa sana au kidogo sana, yote hayo husababisha mazingira muafaka kwa ukuaji wa ugonjwa huu. Viinimbegu vinahitaji maji ili kuota. Viinimbegu hivi husambaa kwenye miti mingine kupitia mvua inayomwagika au kwa njia ya upepo. Ugonjwa wa Doa-jani la Mwani hutumia maji na madini ya chumvi ya mimea inayohifadhi vimelea vyake, na hivyo ugonjwa huu kutambulika kama kupe wa maji au mnyonya maji. Ukuaji wa kuvu hufunika majani hadi yanapukutika. Wadudu wachanga waliopo upande wa juu wa majani wanaweza kuoshwa kabisa (kuondolewa) kwa mvua za mara kwa mara. Ni vile viinimbegu vinavyopenya majani kupitia majeraha tu ndivyo husababisha vidonda. Hakuna ushahidi kwa upenyaji kupitia utando usio na jeraha.


Hatua za Kuzuia

  • Hakikisha kunakuwa na upitishaji mzuri wa hewa kwa kuelekeza mistari ipasavyo.
  • Boresha hali ya ukuaji ili kupunguza athari zinazotokana na mazingira yasiyo rafiki (upungufu wa maji, ukame, n.k) kwa ukuaji wa mimea.
  • Epuka udongo wenye maji mengi kwa kuboresha mfumo wa utoaji maji shambani.
  • Mwagilia maji mapema asubuhi ili kuhakikisha majani yanakauka haraka.
  • Epuka umwagiliaji wa maji kutokea juu kadri inavyowezekana.
  • Ongeza mbolea za madini kunapokuwa na ukuaji duni.
  • Tumia dawa za kupulizia zenye potasiamu fosfeti.
  • Hakikisha msongamano wa mimea unaruhusu mzunguko wa hewa ili kuwezesha ukaukaji haraka wa majani na matunda.
  • Ondoa magugu yaliyo karibu na kuzunguka miti ili kupunguza ushindani wa virutubisho na unyevu kati ya mimea na magugu.
  • Epuka majeraha yanayosababishwa na zana za kilimo.

Pakua Plantix