Boron Deficiency
Upungufu wa Virutubisho
Dalili hutofautiana, kulingana na zao na hali za ukuaji, lakini kwa ujumla huonekana kwanza kwenye ukuaji mpya. Ishara ya kwanza kwa kawaida ni kubadilika rangi na unene wa majani machanga. Rangi ya njano inaweza kuwa sawia, au iliyo fifia katikati ya mishipa ikiwa mbali kidogo kutoka kwenye mishipa mikuu. Majani na shina karibu na ncha ya chipukizi hukakamaa na huvunjika kwa urahisi inapopindishwa. Majani yanaweza kupauka (mpauko ulio kusanyika kidogo kwenye sehemu za katikati ya mishipa) na ncha na sehemu za pembeni zinaweza kujikunja. Wakati mwingine, mishipa ya majani inaweza kuonekana kuwa minene na kuongezeka na vikonyo vinaweza kujisokota. Pingili zinaweza kuwa fupi, na kufanya msongamano mkubwa wa majani karibu na ncha ya juu ya mmea. Katika hatua mbaya zaidi, upungufu wa boroni husababisha kufa kwa seli kwenye sehemu za ukuaji. Mizizi ya kuhifadhia chakula mara nyingi huwa mifupi na yenye ncha butu na huweza kugawanyika kadiri upungufu unavyozidi.
Hakikisha una udongo wenye afya na wenye kiwango kizuri cha maozea/mabaki ya viumbe hai na uwezo mzuri wa kuhifadhi maji kwa kutumia samadi.
-Tumia mbolea zenye boroni (B). - Mfano: disodium octaborate tetrahidrati (Boroni 20%) kunyunyizia majani. - Wasiliana na mshauri wako wa kilimo ili kujua bidhaa bora na kipimo kwajili ya udongo na mazao yako. Mapendekezo Zaidi: - Inashauriwa kupima udongo kabla ya msimu wa kupanda mazao kuanza ili kuboresha uzalishaji wako wa mazao. - Ni vizuri kuweka boroni kwenye udongo kwa sababu dawa za kupulizia majani zinaweza kuharibu majani kwenye mazao mengi.
Upungufu wa boroni kawaida huonekana katika udongo wenye pH ya juu kwa sababu katika hali hii madini haya huwa katika muunganiko wa kemikali ambao si rahisi kwa mmea kuyapata. Udongo wenye kiasi cha chini cha mabaki ya viumbe hai (<1.5%) au udongo wa kichanga (unaokabiliwa na uchujaji wa virutubisho) pia huathirika na upungufu wa boroni. Uwekaji wa boroni hauwezi kurekebisha upungufu katika hali hivyo kwa sababu inaweza isiwe rahisi kufyonzwa na mimea. Dalili kwenye majani zinaweza kufanana na magonjwa mengine: utitiri buibui , upungufu wa zinki au upungufu wa kati wa madini chuma . Kwenye mizizi ya kuhifadhia chakula, uvimbe unaofanana na malengelenge na kupasuka pia yanaweza kuwa dalili za funza(sota) wa kukata mizizi au mabadiliko ya haraka ya unyevu wa udongo. Upungufu wa kalsiamu pia unaweza kusababisha kufa kwa ncha za machipukizi na mizizi, lakini majani machanga chini ya ncha ya chipukizi haya ongezeki unene na hayapati rangi ya njano kati ya mshipa.