Mahindi

Upungufu wa Zinki

Zinc Deficiency

Upungufu wa Virutubisho

Kwa Ufupi

  • Majani kuwa na rangi ya njano, kuanzia kwenye kingo.
  • Mshipa mkuu wa majani hubakia na rangi ya kijani.
  • Kukusanyika kwa majani yaliyoharibika umbo kuzunguka shina.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

31 Mazao

Mahindi

Dalili

Dalili za upungufu wa zinki hutofautiana kati ya spishi moja na nyingine, lakini athari kadhaa zinaweza kujumlishwa. Spishi nyingi huonyesha kubadilika kwa rangi ya majani na kuwa ya njano, mara nyingi huku mshipa mkuu wa majani ukibaki na rangi ya kijani. Katika baadhi ya spishi, majani machanga ndiyo yanayoathiriwa zaidi, lakini kwa spishi zingine, majani mapya na ya zamani yote huoneesha dalili. Majani mapya mara nyingi huwa madogo na membamba zaidi na huwa na kingo zenye milima na mabonde mithili ya mawimbi. Kadri ya muda unavyoenda, madoa ya manjano (klorotiki) yanaweza kubadilika na kuwa na rangi ya shaba nyeusi na madoa yanayotokana na kufa kwa tishu za jani (nekrotiki) yanaweza kuanza kuonekana kutoka kwenye kingo za jani. Katika baadhi ya mazao, majani yenye upungufu wa zinki mara nyingi vifundo hukaribiana , na hivyo majani hukusanyika kwenye shina. Kuharibika kwa umbo la jani na kupungua kwa ukuaji kunaweza kutokea, unaosababishwa na ukuaji duni wa majani mapya (majani yaliyodumaa) na umbali mfupi kati ya kifundo na kifundo.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kutumia samadi asilia kwenye kitalu au shambani siku chache baada ya kupandikiza husaidia kupunguza uwezekano wa kutokea upungufu wa zinki.

Udhibiti wa Kemikali

  • Tumia mbolea yenye zinki (Zn).
  • Kwa mfano: Mbolea ya Salfeti ya Zinki (ZnSO4) kwa kawaida hutumiwa kwa kupulizia majani.
  • Shauriana na mshauri wako wa kilimo ili kujua bidhaa bora na kipimo sahihi kwa udongo na mazao yako.

Mapendekezo zaidi:

  • Inashauriwa kupima udongo kabla ya kuanza msimu wa kupanda ili kuboresha uzalishaji wa mazao yako.
  • Matumizi ya zinki kwenye udongo yanapaswa kufanyika kabla ya kupanda.
  • Kuchovya mbegu kwenye zinki kunaweza kutoa virutubisho kwa mazao.

Ni nini kilisababisha?

Upungufu wa zinki ni tatizo kubwa hasa kwenye udongo wa mchanga wenye alikali (pH ya juu) ambao una kiwango kidogo cha mabaki ya viumbe hai. Viwango vya juu vya fosforasi na kalsiamu kwenye udongo (udongo wa chokaa) pia vinaathiri upatikanaji wa zinki kwa mimea. Kwa kweli, matumizi ya fosforasi yanaweza kuonyesha athari mbaya kwenye unyonyaji wa zinki. Uongezaji wa malighafi zenye kalsiamu kama vile chokaa pia usawazisha kiwango cha asidi ya udongo hupunguza unyonyaji wa zinki kwa mimea (hata kama viwango kwenye udongo hubaki bila kubadilika). Upungufu wa zinki pia unaweza kuwa tatizo wakati udongo umepoa na una unyevunyevu wakati wa hatua ya ukuaji wa mimea.


Hatua za Kuzuia

  • Tumia samadi asilia kabla ya kupanda mbegu au kupandikiza.
  • Usitumie chokaa kwenye udongo kwani hii huongeza pH na kuzuia unyonyaji wa zinki.
  • Chagua aina za mimea zinazovumilia upungufu wa madini ya zinki au zenye uwezo mzuri wa kupata zinki kutoka kwenye udongo.
  • Tumia mbolea zenye mchanganyiko wa zinki.
  • Tumia mbolea zinazotokana na urea (zinazozalisha hali ya asidi) badala ya zile zinazotokana na salfeti ya amonia.
  • Hakikisha hutumii mbolea ya fosforasi kupita kiasi.
  • Mara kwa mara fuatilia ubora wa maji ya umwagiliaji.
  • Ruhusu mashamba yaliyofurika maji kuondosha maji hayo na kukauka kila baada ya muda fulani.

Pakua Plantix