Manganese Deficiency
Upungufu wa Virutubisho
Dalili ni ndogo kuliko upungufu mwingine wa virutubisho na hutegemea sana zao husika. Mishipa ya majani ya kati na ya juu (machanga) ya mimea yenye upungufu wa manganese hubakia ya kijani huku sehemu iliyobaki ya jani kwanza inakuwa ya kijani mpauko, kisha hutengeneza muundo wa madoadoa wa rangi ya kijani mpauko hadi manjano (interveinal chlorosis). Baada ya muda, vidonda vidogo vidogo vyenye seli mfu hukua kwenye tishu zilizo badilika rangi, haswa karibu na kingo na ncha (kuungua kwa ncha). Kupungua kwa ukubwa wa jani, kuharibika umbo na kujinja kwa kingo za majani ni dalili nyingine zinazowezekana. Isiporekebishwa, madoa ya rangi ya kahawia yenye tishu zilizo kufa yanaweza kutokea kwenye nyuso za majani, na majani yaliyoathiriwa sana hubadilika kuwa kahawia na kunyauka. Hupaswi kufananisha na upungufu wa Magnéziamu, ambao dalili zake ni sawa lakini hujitokeza kwanza kwenye majani ya zamani/makongwe.
Tumia samadi, matandazo ya asili au mboji kusawazisha kiasi cha virutubisho na pH ya udongo. Hivi vina mabaki ya viumbe hai ambayo huongeza kiwango cha maozea kwenye udongo na uwezo wake wa kutunza maji na kupunguza pH kidogo.
Mapendekezo Zaidi:
Upungufu wa Manganizi (Mn) ni tatizo lililoenea sana, mara nyingi hutokea kwenye udongo wa kichanga, udongo wa kikaboni wenye pH zaidi ya 6 na udongo ulio athiriwa sana na mmomonyoko, udongo wa kitropiki. Kinyume chake, udongo wenye tindikali nyingi huongeza upatikanaji wa madini haya. Matumiazi ya mbolea kupita kiasi au yasio na uwiano yanaweza kusababisha baadhi ya virutubisho vidogo kushindana ili kupatikana kwa mmea. Mn ina jukumu muhimu katika usanisinuru na unyambulishaji wa naitreti. Kama chuma, boroni na kalsiamu, manganizi haiwezi kuzunguka ndani ya mmea, hujilimbikiza kwenye majani ya chini. Hii inaelezea kwanini dalili huonekana kwanza kwenye majani machanga. Mazao yanayoonyesha uwezekano mkubwa wa upungufu wa Mn na mwitikio chanya wa kurutubishwa na kirutubisho hiki ni: nafaka, kunde, matunda ya jamii ya fyulisi, mazao ya mitende, machungwa, viazi-sukari na kanola, miongoni mwa wengine.