Iron Deficiency
Upungufu wa Virutubisho
Dalili za upungufu wa madini ya chuma huonekana kwanza kwenye majani machanga. Dalili hujulikana kwa umanjano (chlorosis) wa majani ya juu, na mishipa ya katikati na mishipa ya majani iliyobaki wazi ya kijani (chlorosis inayotokea katikati ya mishipa). Katika hatua za baadaye, ikiwa hakuna hatua zinazochukuliwa, jani lote hubadilika kuwa na rangi mithili ya nyeupe-njano na madoa ya kahawia yanayotokana na kufa kwa tishu huanza kuonekana kwenye ubapa wa jani, mara nyingi husababisha ukuaji wa mabaka kwenye ukingo wa jani kutojana na kufa kwa tishu. Maeneo yaliyoathiriwa yanaweza kutambuliwa kwa urahisi kutokea mbali ya shamba. Mimea yenye upungufu wa madini ya chuma imedumaa katika ukuaji na inaweza kutoa mavuno kidogo.
Wakulima wadogo wanaweza kutumia mbolea ya majani iliyotengenezwa na majani ya upupu na mwani iliyokamuliwa. Uwekaji wa samadi ya wanyama na mboji pia huongeza chuma kwenye udongo. Panda mchunga karibu na mazao yako, kwa vile hufanya chuma kupatikana kwa mazao ya karibu, hasa miti.
Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuwa tatizo kubwa katika udongo wa kitropiki uliovuja au kwenye udongo usiopenyesha maji vizuri, hususani chini ya chemchemi za baridi na unyevunyevu. Mtama, mahindi, viazi na maharagwe ndiyo mazao yaliyoathiriwa zaidi na ngano pamoja na alfa alfa ndiyo yasiyoathirika sana. Udongo wenye madini ya chokaa, alkali (pH 7.5 au zaidi) inayotokana na mawe ya chokaa hufanya mimea kukabiliwa na upungufu wa madini ya chuma. Chuma ni muhimu kwa usanisinuru (yaani mchakato wa mimea kutumia mwanga wa jua,maji na hewa ukaa), ukuzaji, na udumishaji wa vifundo vya mizizi kwenye mazao jamii ya mikunde. Kwa hivyo, upungufu wa madini ya chuma hupunguza sana wingi wa vifundo, uwezo ubadilishaji wa naitrojeni kuweza kutumika na mimea, na pia hupunguza mavuno ya mazao. Kiwango muhimu kinachokadiriwa ni karibu 2.5 mg/kg ya tishu kavu ya mmea. Upungufu wa chuma pia huongeza uchukuaji na mkusanyiko wa cadimi (kadimi) kwenye mimea.