Karanga

Upungufu wa Naitrojeni

Nitrogen Deficiency

Upungufu wa Virutubisho

Kwa Ufupi

  • Ubadilikaji rangi wa majani - kijani iliyopauka, vikonyo vya rangi nyekundu iliyofifia na vijishipa.
  • Ukuaji uliodumaa wa majani.
  • Mwonekano mrefu na mwembamba wa mmea.

Inaweza pia kupatikana kwenye

58 Mazao
Mlozi
Tufaha
Aprikoti
Ndizi
Zaidi

Karanga

Dalili

Dalili hujitokeza kwanza kwenye majani ya zamani na huenda hatua kwa hatua hadi kwa majani machanga. Katika hali ambayo tatizo ni dogo, majani ya zamani yaliyokomaa yanageuka kuwa na rangi ya kijani iliyopauka. Ikiwa haijarekebishwa, baada ya muda ueneaji wa umanjano unakua kwenye majani hayo pamoja na kubadilika kwa rangi nyekundu iliyofifia ya vishipajani na vikonyo. Kadiri upungufu wa naitrojeni unavyoendelea, majani haya hatimaye yanageuka na kuwa ya manjano-nyeupe (ikijumuisha vishipajani) na yanaweza kujikunja au kuharibika umbo. Majani machanga yanabaki kuwa ya kijani iliyopauka lakini hukua na kuwa madogo zaidi kuliko kawaida. Mimea huonekana kuwa mirefu na myembamba kutokana na kupungua kwa uwezo wa kuzalisha matawi lakini urefu wake ni wa kawaida. Mimea inakuwa kwenye hatari ya kuathirika zaidi kunapokuwa na mahitaji makubwa ya maji kuliko yaliyopo na kunyauka kwa majani ni kawaida. Kifo cha mapema na kupukutika kwa mjani kunaweza kutokea, na hivyo kusababisha kupungua kwa mavuno. Urejeaji wa hali ya kawaida unaonekana dhahiri baada ya siku chache za matumizi ya mbolea ya naitrojeni.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Viwango vya juu vya maada asilia (yaani mabaki ya viumbe hai) katika udongo vinaweza kuimarisha muundo wa udongo na kuboresha uwezo wa udongo kuhifadhi maji na virutubisho. Maada asilia au mabaki ya viumbe hai yanaweza kuongezwa kwenye udongo kama samadi, mboji, au kwa kuongeza mbolea iliyotengenezwa na majani ya upupu, vinyesi vya ndege wa baharini na vya popo, unga uliotengenezwa kutokana na pembe na/au kwato za ndani au nitrolime. Mbolea iliyotengenezwa kwa majani ya upupu inaweza kunyunyiziwa moja kwa moja kwenye majani.

Udhibiti wa Kemikali

  • Tumia mbolea zenye naitrojeni (N).
  • Mifano: Urea, NPK, naitreti ya ammoniamu.
  • Wasiliana na mshauri wako wa kilimo ili kujua bidhaa bora za mbolea na dozi kwa ajili ya udongo na mazao yako.

Mapendekezo Zaidi:

  • Inapendekezwa kupima udongo kabla ya msimu wa kupanda mazao kuanza ili kuboresha uzalishaji wako wa mazao.
  • Bora zaidi kuweka mbolea ya naitrojeni katika migawanyiko mingi katika msimu mzima.
  • Usitumie ikiwa unakaribia wakati wa kuvuna.

Ni nini kilisababisha?

Viwango vya juu vya naitrojeni ni muhimu wakati wa ukuaji wa mmmea. Katika nyakati za hali ya hewa nzuri, ni muhimu kutoa usambazaji mzuri wa naitrogeni kwa mazao yanayokua haraka ili yaweze kufikia uwezo wao wa juu wa kuzalisha mimea na matunda/nafaka. Upungufu wa naitrojeni unaweza kuonekana katika udongo wa kichanga, unaopitisha maji vizuri ukiwa na maada/mata ogania (viumbe hai) kidogo kwa vile huathiriwa na uchujaji wa virutubisho. Mvua za mara kwa mara, mafuriko au umwagiliaji mkubwa huosha naitrojeni na kuizamisha kwenye udongo na pia inaweza kusababisha upungufu. Vipindi vya upotevu wa maji (kwa njia ya uvukizaji/mvukizo) kutokana na ukame huzuia ufyonzaji wa maji na virutubisho, na hivyo kusababisha ugavi wa virutubisho usio na uwiano. Hatimaye, pH ya udongo pia ina jukumu katika upatikanaji wa naitrojeni kwenye mmea. pH ya udongo, ya chini au ya juu zote huathiri vibaya ufyonzaji wa naitrojeni wa mmea.


Hatua za Kuzuia

  • Angalia pH ya udongo na chokaa ili kupata kiwango muafaka kabla ya kuanza kwa msimu wa kupanda ili kuboresha uzalishaji wako wa mazao.
  • Wezesha shamba na mfumo mzuri wa utoaji maji na usimwagilie kupita kiasi.
  • Utumiaji wa mbolea uliopitiliza au usio na uwiano unaweza kusababisha baadhi ya virutubisho kutopatikana kwa mmea.
  • Hakikisha unamwagilia mimea mara kwa mara wakati wa ukame.
  • Hakikisha umeongeza vitu asilia au mabaki ya viumbe hai kutoka kwenye mboji, samadi au matandazo kwa mfano.
  • Uchanganuzi wa vikonyo unaweza kuruhusu wakulima kugundua mwisho wa upungufu wa naitrojeni kwenye mazao.

Pakua Plantix