Phosphorus Deficiency
Upungufu wa Virutubisho
Dalili za upungufu wa fosforasi zinaweza kuonekana katika hatua zote za ukuaji wa mimea lakini zinajitokeza zaidi kwenye mimea michanga. Tofauti na virutubisho vingine, dalili za upungufu huu hazionekani kwa urahisi na zinaweza kuwa ngumu kuzitambua. Katika hali ambayo tatizo ni dogo, ishara inayoweza kuonekana kwa tatizo hili ni kwamba, mimea inakuwa mifupi au inadumaa. Hata hivyo, hakuna dalili za wazi zinazojitokeza kwenye majani. Inapotokea kuwa na upungufu mkubwa wa fosfarasi, shina na vikonyo hubadilika rangi zake za asili na kuonesha rangi ya kijani kibichi hadi zambarau. Sehemu za chini za majani ya zamani pia zinaonyesha rangi ya zambarau, kuanzia kwenye ncha na kingo, na baadaye kusambaa kwenye uso wote wa jani. Majani yanaweza kuwa na mguso mgumu mithili ya ngozi na mishipa ya jani inaweza kutengeneza muonekano mithili ya wavu wenye rangi ya kahawia. Katika mazingira fulani, upungufu wa fosforasi unajulikana kwa uwepo wa ncha zilizoungua na majani kugeuka kuwa ya manjano na utokeaji wa mabaka yanatokana na kufa kwa tishu kwenye kingo za majani. Maua na matunda yanazalishwa, lakini mavuno ya matunda ni kidogo.
Viwango vya fosforasi kwenye udongo vinaweza kurejeshwa kwa kutumia samadi ya shambani, au vitu vingine (matandazo ya kikaboni, mboji na vinyesi vya ndege wa baharini) au mchanganyiko wa hivyo vitu. Uchanganyaji wa mabaki ya mazao kwenye udongo baada ya mavuno unaweza pia kuchangia kudumisha uwiano mzuri wa fosforasi katika muda mrefu na kuboresha muundo wa udongo. Uozo wa vitu vya kikaboni hutoa fosforasi kwa mimea kwa njia endelevu.
Mapendekezo zaidi:
Kuna tofauti ya uwezekano wa kupata upungufu wa fosforasi kwa mazao mbalimbali. Mizizi hufyonza ioni (molekuli yenye chaji ya umeme) za fosfeti wakati zinapoyeyushwa kwenye maji maji ya kwenye udongo. Udongo wenye chokaa na viwango vya juu vya kalsiamu unaweza kuwa na upungufu wa fosforasi. Hata hivyo, kwa kawaida, kikwazo ni uwepo wa kirutubisho hiki kwa sababu fosforasi inashikamana kwenye chembe chembe za udongo na haiwezi kufyonzwa na mmea. Udongo wa alkali na wa tindikali unaweza kuonyesha upatikanaji mdogo wa fosforasi. Udongo wenye kiwango kidogo cha vitu vya kikaboni (vitu vinavyoweza kuoza) au udongo wenye chuma nyingi pia unaweza kuwa ni tatizo. Hali ya hewa ya baridi inayozuia ukuaji na ufanyaji kazi mzuri wa mizizi inaweza pia kusababisha tatizo hili. Hali ya ukame au magonjwa yanayozuia mizizi kufyonza maji na virutubisho vinaweza kusababisha dalili za upungufu. Kwa upande mwingine, unyevu wa udongo huongeza ufyonzaji wa kirutubisho hiki na kusababisha mavuno mengi zaidi.