Magnesium Deficiency
Upungufu wa Virutubisho
Mimea yenye upungufu wa magneziamu/magnesi kwa kawaida huonyesha muundo wa madoa ya rangi ya kijani iliyopauka au yaliyobadilika rangi na kuwa ya manjano katikati ya tishu za majani ya zamani, mara nyingi huanzia karibu na ukingo. Kwenye nafaka, majani yenye upungufu mdogo huonyesha mistari ya kijani mithili ya shanga ambayo inaendelea hadi kwenye vishipa vya katikati vilivyobadilika rangi na kuwa vya manjano. Katika hali mbaya, kuendelea kwa rangi ya manjano kuelekea katikati ya jani na mishipa midogo pia huathirika. Madoa mekundu au ya kahawia huonekana kwenye sehemu bapa ya jani. Baadaye, maendeleo ya maeneo yaliyokufa tishu kwenye sehemu ambazo kuna ubadilikaji mkubwa wa rangi ya tishu kutoka kijani hadi manjano hufanya majani kuwa yenye makunyanzi na kuharibika umbo. Mwishowe, rangi ya manjano hufunika jani lote, na hatimaye husababisha kufa na kupukutika kabla ya wakati. Ukuaji wa mizizi hudumaa, na kusababisha mmea kuwa dhaifu.
Tumia vitu vyenye magnesi kama vile chokaa ya mwani, dolomite au chokaa yenye magnesi. Tumia samadi, matandazo ya asili au mboji ili kusawazisha kiasi cha virutubisho kwenye udongo. Hivyo vyote vina vitu vya kikaboni na virutubisho vingi ambavyo hutolewa polepole kwenye udongo.
Mapendekezo zaidi:
Upungufu wa magneziamu/magnesi ni tatizo la kawaida katika udongo mwepesi, kichanga, au wa asidi wenye uwezo mdogo wa kuhifadhi virutubisho na maji. Katika udongo huo, virutubisho vinaweza kuoshwa kwa urahisi. Udongo wenye potasiamu nyingi au amonia au uwekaji wa ziada wa virutubisho hivi unaweza pia kuwa tatizo kwa sababu virutubisho hivi hushindana na magneziamu katika udongo. Magneziamu inahusika katika usafirishaji wa sukari na ni sehemu muhimu ya molekyuli za klorofili. Bila kiwango cha kutosha cha magneziamu, mimea huanza kupunguza uwezo wa klorofili katika majani ya zamani ili kuhamishia kwenye majani mapya yanayokua. Hii inaelezea utokeaji wa rangi ya manjano kati ya vishipa vya majani. Nguvu ya mwanga inaathiri utokeaji wa dalili hizi. Mwanga mkali huzorotesha athari za upungufu.