Tufaha

Upungufu wa Kalisi (Madini Chokaa)

Calcium Deficiency

Upungufu wa Virutubisho

Kwa Ufupi

  • Madoa ya manjano yasiyo na mpangilio kwenye majani.
  • Majani yaliyojikunja.
  • Machipukizi au shina na matunda machanga yaliyokua vibaya.
  • Mmea kunyauka.
  • Ukuaji uliodumaa.

Inaweza pia kupatikana kwenye

59 Mazao
Mlozi
Tufaha
Aprikoti
Ndizi
Zaidi

Tufaha

Dalili

Dalili hizi zinaonekana hasa kwenye sehemu zinazokua haraka kama vile machipukizi mapya na majani. Ukuaji mbaya wa machipukizi machanga na baada ya muda idadi yake hupungua. Mwanzoni, majani mapya au ya kati yanaweza kuonyesha madoa ya klorotiki yaliyotawanyika kwa nasibu kwenye kipande. Ikiwa haitashughulikiwa, huanza kujikunja chini au juu na kingo zake zinakuwa na hali ya seli zilizo kufa na ya kuungua. Majani yaliyo komaa na ya zamani kwa ujumla hayathiriwi. Mfumo wa mizizi hukua vibaya na mimea ina tabia ya kunyauka na kuonyesha ukuaji uliodumaa. Kwa upungufu mkubwa, maua yanaweza kudondoka, na sehemu ya kukua ya majani mapya huonekana kama imeungua au kufa kabisa. Matunda ni madogo na hayana ladha, na kwa matango, pilipili na nyanya yanaweza kuoza kwenye ncha ya matunda. Mbegu huwa na kiwango cha chini cha uotaji.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Kwa wakulima wadogo au bustani, maganda ya mayai yaliyosagwa vizuri na kuchanganywa na asidi dhaifu (siki) inaweza kutumika. Vinginevyo, tumia vitu vyenye kalisi kama chokaa ya mwani, unga wa basalt, chokaa iliyochomwa, dolomite, jasi, na chokaa ya slag. Vitu asilia kama samadi au mboji vinaweza kuongezwa kwenye udongo ili kuboresha uwezo wake wa kuhifadhi unyevu.

Udhibiti wa Kemikali

  • Tumia mbolea za udongo zenye kalsiamu (Ca).
    • Mifano: Kalsiamu naitreti (CAN), chokaa, jasi.
    • Wasiliana na mshauri wako wa kilimo kujua bidhaa bora na kipimo sahihi kwa udongo na zao lako.

Mapendekezo zaidi:

  • Inashauriwa kufanya kipimo cha udongo kabla ya msimu wa kupanda ili kuboresha uzalishaji wa mazao yako.
  • Kalsiamu naitreti muyeyuko ni mbolea ya kunyunyiza majani kwa upungufu uliopo.
  • Unapotumia kalsiamu kloraidi, usipulize kama joto liko juu ya 30°C.
  • Wakati wa maandalizi ya shamba, tumia chokaa ikiwa pH ya udongo ni tindikali na tumia jasi ikiwa pH ya udongo ni alkali.
  • Kuweka chokaa kunaweza kufanyika miezi miwili hadi minne kabla ya kupanda.

Ni nini kilisababisha?

Dalili hizi kwa ujumla zinahusiana na upatikanaji wa virutubisho hivi kwa mmea kuliko upungufu wa kwenye udongo. Kalsiamu haisafiri ndani ya mmea na unyonyaji wake unahusiana sana na unyonyaji na usafirishaji wa maji kwenye mmea. Hii inaeleza kwanini majani mapya yanaonyesha dalili za upungufu kwanza. Udongo mzito na udongo unaonyeshewa vizuri ni mzuri kwa kuyeyusha kalsiamu na kuileta kwenye mmea. Hata hivyo, udongo wa mchanga, wenye uwezo mdogo wa kuhifadhi maji, huwa na uwezekano wa ukame na unaweza kuzuia unyonyaji wake. Kuacha udongo ukauke sana kabla ya kumwagilia maji pia kunaweza kusababisha dalili hizi. Udongo wenye pH ya chini, chumvi nyingi au udongo wenye amonia nyingi pia unaweza kuwa na tatizo. Unyevunyevu mwingi wa hewa au udongo uliopo kwenye mafuriko unaweza kupunguza usafirishaji wa maji kwenye tishu, na hivyo kalsiamu kidogo kunyonywa.


Hatua za Kuzuia

  • Chagua aina ambazo zina uwezo mzuri wa kufyonza kalsiamu kutoka kwenye udongo.
  • Hakikisha unapima pH ya udongo na kuongeza chokaa ikiwa ni lazima ili kufikia kiwango bora kati ya 7.0 na 8.5.
  • Punguza matumizi ya mbolea za ammoniamu ili kuepuka upungufu wa kalsiamu kwenye udongo.
  • Usitumie mbolea nyingi za naitrojeni wakati wa ukuaji wa mapema wa matunda.
  • Kuwa mwangalifu usiumize mizizi wakati wa kufanya kazi karibu na mimea.
  • Hakikisha kumwagilia mara kwa mara, lakini usimwagilie kupita kiasi.
  • Ongeza vitu vya asili/kikaboni kwenye udongo, kwa mfano, samadi au matandazo ya asili au mboji.
  • Matandazo ya kijani (nyasi kavu, vumbi la mbao lililooza) au matandazo ya plastiki yanaweza kusaidia udongo kuhifadhi unyevu.
  • Fuatilia shamba mara kwa mara na uondoe matunda yenye dalili.

Pakua Plantix