Potassium Deficiency
Upungufu wa Virutubisho
Dalili huonekana zaidi kwenye majani ya zamani na huanza tu kujitokeza kwenye majani machanga ikiwa kuna upungufu mkubwa wa madini ya potasiamu. Upungufu wa wastani wa potasiamu unatambulika kwa kujitokeza rangi ya manjano kiasi kwenye kingo na ncha za majani, kisha kufuatiwa na kuungua kwa ncha. Sehemu bapa ya jani (lamina) inabadilika rangi na kuwa iliyo pauka kwa kiasi fulani lakini mishipa mikuu inabaki kuwa ya kijani kibichi (umanjano katikati ya mishipa). Ikiwa hayatafanyika marekebisho, mabaka haya (yanayotokana na majani kubadilika rangi) hatimae hubadilika na kuwa mithili ya ngozi kavu ya kahawia ya manjano au kahawia nyeusi (kufa kwa tishu) ambayo kwa kawaida huendelea kutoka kwenye pembe ya jani hadi kwenye mshipa wa kati wa jani; yaani vena kuu. Hata hivyo, mishipa mikuu huwa na tabia ya kubaki ya kijani. Majani hupinda na kujisokota na mara nyingi hudondoka mapema. Majani machanga huwa madogo na dhaifu, yakichukua muonekano wa kikombe. Mimea yenye upungu wa potasiamu hudumaa na huathirika zaidi na magonjwa na changamoto zingine kama ukame na baridi kali. Katika hali zingine, matunda yanaweza kuharibika vibaya.
Ongeza mbolea za asilia kama majivu au majani ya mimea kwenye udongo angalau mara moja kwa mwaka. Majivu ya kuni pia huwa na kiwango kikubwa cha potasiamu. Kutumia chokaa kwenye udongo wenye tindikali kunaweza kuongeza utunzaji wa potasiamu kwenye aina fulani za udongo kwa kupunguza uchujaji/upoteaji wa virutubisho.
Mapendekezo zaidi:
Upungufu unaweza kutokea kutokana na akiba ndogo ya potasiamu katika udongo au upatikanaji mdogo kwenye mimea. Udongo wenye pH ya chini na udongo wenye mchanga au udongo mwepesi wenye kiwango kidogo cha maozea ya viumbe hai huwa kwenye hatari ya kuvujisha virutubisho na ukame, na kwa hiyo kuweza kusababisha matatizo. Umwagiliaji kupita kiasi na mvua nyingi huosha/huondoa virutubisho kutoka kwenye eneo la mizizi na pia inaweza kusababisha upungufu. Joto kali au hali ya ukame huzuia usafirishaji wa maji na virutubisho kwenye mimea. Viwango vikubwa vya fosforasi, magnesiamu, na madini ya chuma pia vinaweza kushindana na potasiamu. Potasiamu ina jukumu muhimu katika usafirishaji wa maji, ukakamavu wa tishu, na ubadilishanaji wa gesi na angahewa. Dalili za upungufu wa potasiamu haziwezi kurekebishwa, hata kama potasiamu itaongezwa baadaye kwenye mimea.