Tikiti

Kuoza Kitako

Calcium Deficiency Rot

Upungufu wa Virutubisho

Kwa Ufupi

  • Madoa ya kahawia au kijivu chini ya matunda mabichi.
  • Uozo mweusi wa ndani kwenye matunda.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Tikiti

Dalili

Ugonjwa wa Kuoza Kitako unajulikana kwa kuonekana kwa doa lisilo la kawaida kwenye ncha ya tunda. Doa hili huwa na ukubwa na rangi tofauti. Katika hatua za awali, doa linakuwa la kijani hafifu/nyepesi. Doa hilo hubadilika na kuwa kahawia na jeusi kadri tunda linavyokomaa. Tishu za tunda hupoteza uthabiti, zinakuwa zimezama, na ncha hatimaye huonekana kama imetandazwa. Uozo mweusi wa ndani pia unaweza kutokea kwenye matunda huku uozo huo ama ukionesha dalili chache au kutoonesha dalili zinazoonekana kwa nje.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Weka kwenye udongo vitu vyenye kalsiamu nyingi, na vitu hivi ni kama vile chokaa ya mwani, unga wa gumawesi (basalt), chokaa iliyochomwa, dolomite, jasi, na chokaa ya taka za mawe.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu zinazojumuisha hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia, ikiwa yanapatikana. Tumia dawa ya kupulizia majani yenye kalsiamu kloridi kama hatua ya dharura, lakini usipulizie mara nyingi au kwa kiasi kikubwa.

Ni nini kilisababisha?

Uozo wa Kitako ni tatizo la kimaumbile linalosababishwa na upungufu wa madini ya kalsiamu kwenye tishu za matunda. Hakuna wadudu waharibifu au vimelea vya magonjwa vinavyohusika. Madini ya Kalsiamu husaidia kuimarisha na kufanya tishu ziwe thabiti. Upungufu wa kalsiamu unaweza kutokea kutokana na ukosefu wa virutubisho hivi kwenye udongo au mmea kushindwa kuvifyonza virutubisho hivyo na kuvisambaza kwenye matunda yake. Hii husababisha uharibifu wa umbile la tishu, na kusababisha maeneo yenye rangi nyeusi, yaliyozama. Umwagiliaji usio wa mara kwa mara au uharibifu wa mizizi unaweza kuwa chanzo cha upungufu wa kalsiamu.


Hatua za Kuzuia

  • Rekebisha viwango vya alkali na tindikali ya udongo (yaani, pH ya udongo), kwa mfano kwa kutumia chokaa.
  • Tumia matandazo ili kutunza unyevu nyevu wa udongo.
  • Epuka kuharibu/kukata mizizi kupitia mbinu za kulima katika kina kirefu cha udongo.
  • Hakikisha uwekaji wa mbolea yenye kiwango kidogo cha naitrojeni na yenye kalsiamu nyingi.
  • Hakikisha umwagiliaji wa mara kwa mara wakati wa vipindi vya ukame.
  • Epuka umwagiliaji wa kupita kiasi na hakikisha kunakuwa na mfumo mzuri wa utoaji maji shambani.
  • Tumia aina za naitrojeni zenye naitreti badala ya amonia.

Pakua Plantix