Hyposidra talaca
Mdudu
Kwanza, viwavi wadogo hula sehemu laini ya majani, hivyo kuifanya ionekane kama ganda jembamba, linaloweza kupitisha mwanga. Kadri viwavi hawa wanavyokua, hula majani mazima kuanzia kwenye sehemu ya nje hadi kuingia sehemu ya katikati ya kichaka cha chai. Ikiwa kama idadi yao ni kubwa, basi wanaweza kumaliza kabisa majani yote yaliyopo kwenye vichaka vya chai. Hivyo kuvifanya vichaka hivi kuonekana kuwa tupu na katika hali ya kuungua. Majani yanapoliwa tena na tena, kichaka cha chai huzidi kudhoofika, ubora wa chai iliyovunwa hupungua, na mimea hushambuliwa kwa urahisi zaidi na wadudu na magonjwa mengine.
Wadudu kadhaa wa asili, walio adui wa nondo huyu mweusi, wamepatikana na wanaweza kutumiwa katika mpango jumuishi wa udhibiti wa wadudu (IPM). Nyigu wanyonyaji (k.m. Cotesia ruficrus) hutaga mayi yao ndani ya nondo huyu. Idadi yao huwa kubwa zaidi katika majira ya kuchipua na kupukutika kwa majani, ambayo pia ndio majira ambayo idadi ya nondo hawa huongezeka. Kunguni wawindaji (k.m. Eocanthecona furcellata) hula kiwavi cha nondo huyu na hupatikana kipindi chote cha msimu, lakini huwa wengi zaidi kuanzia Juni hadi Septemba. Adui hawa wa asili wanaweza kukuzwa katika idadi kubwa na kisha kuachiliwa mashambani. Pia, kirusi kinachoitwa Hyposidra talaca nucleopolyhedrovirus (HytaNPV) ni mdudu wa asili anayeonekana kuwa na uwezo wa kuwauwa nondo hawa. Majaribio yaliyofanyika shambani yalionyesha kwamba kutumia mililita 800-1000 kwa hekta kulipunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya nondo hawa. HytaNPV huhesabika kuwa mbadala salama na fanisi wa kemikali za kuuwa wadudu katika programu jumuishi ya udhibiti wa wadudu (IPM).
Daima zingatia kutumia mbinu jumuishi zinazojumuisha mikakati ya kinga sambamba na matibabu ya kiasili, kama ikiwezekana. Kihistoria, udhibiti wa nondo huyu mweusi umetegemea sana dawa za kuuwa wadudu; hata hivyo, hali ya usugu wa aina nyingi za kemikali hizi ni tatizo kubwa na linaloendelea kukua katika kanda kuu zinazolima zao la chai. Badili aina za dawa za kuuwa wadudu mara kwa mara ili kupunguza uundwaji wa usugu zaidi, na daima tumia dawa hizo kama vile ilivyoelekezwa katika lebo.
Uharibifu huu husababishwa na kiwavi cha nondo mweusi, Hyposidra talaca, ajulikanaye pia kama mnyoo mweusi. Nondo huyu mweusi huonekana kama jani lililokauka, hali inayomwezesha kujificha kwa urahisi. Nondo wa kike hutaga makundi makubwa ya mayai (takribani 250) katika eneo la chini la gome lililolegea, katika kuvumwani, ama juu ya mizizi ya miti ya vivuli iliyopo kwenye shamba la chai. Hawatagi mayai moja kwa moja juu ya mimea ya chai. Mayai yanapoanguliwa, viwavi weusi wadogo sana wenye madoa meupe ya umbo la pete hudondoka kutoka kwenye miti ya vivuli na kuanza kuyala majani ya chai. Mdudu huyu huzaa vizazi vingi (6 hadi 8) ndani ya mwaka mmoja, hii ndio maana hupatikana daima katika mimea ya chai. Milipuko ya ugonjwa huu mara nyingi hutokea kipindi cha joto, kipindi miti ya vivuli inapokuwa imestawi, na kipindi dawa nyingi za kuuwa wadudu zinapokuwa zimenyunyizwa kwenye shamba, ambazo huuwa pia wadudu wa asili ambao ni adui wa viwavi hawa. Aidha, mabadiliko ya hali ya hewa inasababisha pia kuwepo kwa milipuko mingi zaidi mara kwa mara katika maeneo yanayolimwa zao la chai karibu na milima ya Himalaya.

This page is powered by millions of live Plantix diagnoses. Build plant-disease detection like this into your own products with the API Toolkit, part of Plantix Intelligence.