Ascia monuste
Mdudu
Dalili za wazi za maambukizi ni wakati majani ya yanapoharibika kutokana na kuliwa. Viwavi wa Vipepeo Weupe wa Kusini Mkuu ndio wanaosababisha uharibifu huu. Kwa kawaida viwavi hula kingo za majani, wakianzia sehemu za nje na kuhamia ndani. Aina hii ya ulaji wa majani mara nyingi hutengeneza matundu yasiyo sawa kando ya kingo za majani. Viwavi wana uwezo wa kula sehemu zote za mimea zilizo juu ya ardhi. Viwavi hawa hula kwa uroho mboga za jamii ya kabichi ambazo ni kabichi, koliflawa, brokoli). Kuwa makini na makundi ya mayai kwenye upande wa juu wa majani na viwavi wanaokula pamoja katika makundi. Unaweza pia kuona nondo kamili shambani.
Fikiria kutumia dawa ya kupulizia ya Bacillus thuringiensis (Bt), ambayo ni dawa ya kuua wadudu inayotokana na kemikali asilia ambayo hulenga na kuua lava wa minyoo ya kabichi huku ikiwa ni salama kwa wanadamu na wadudu wenye manufaa. Tumia mafuta ya kupulizia ya mwarobaini, yanayotokana na mti wa mwarobaini, ambayo hutumika kama dawa asilia ya kufukuza na kuua wadudu.
Daima zingatia mbinu jumuishi na hatua za kinga pamoja na matibabu ya kibaiolojia/matibabu rafiki kwa mazingira. Kwa mujibu wa maandiko mbalimbali, nyingi ya dawa hizi za kuua wadudu, zinadhibiti kwa ufanisi mdudu huyu lakini sio dawa zote ni salama kwa maadui wa asili (yaani wadudu wanaokula wadudu waharibifu akiwemo na mdudu huyu); na dawa hizo ni: Chlorantraniliprole, cyantraniliprole, indoxacarb, spinosad, chlorfenapyr. Aidha, matumizi ya dawa za kuua wadudu yanaweza kusababisha usugu wa wadudu kwa madawa, na hivyo kufanya wadudu kutoathirika sana kadri muda unavyosonga.
Uharibifu huu unasababishwa na viwavi wa mdudu aitwae Kipepeo Mkuu Mweupe wa Kusini(yaani Ascia monuste). Huyu ni mdudu hatari sana anayesababisha hasara kubwa katika mazao ya jamii ya kabichi. Majike hutaga makundi ya mayai yenye rangi ya njano, yenye umbo mithili ya mkono wa kisokotea nyuzi kwenye upande wa juu wa majani. Hii hutokea kati ya mwezi Novemba na Mei, kipindi cha joto na mvua katika maeneo ya tropiki. Viwavi wana rangi ya manjano yenye mistari ya kijivu. Mistari hiyo inaenda sambamba na miili yao na wana madoa madogo ya kahawia. Vipepeo kamili ambao ni madume wana rangi nyeupe na majike wana rangi nyeupe iliyochafuka hadi kijivu. Vipepeo hawa wanaishi kwa takriban siku 19 na watasafiri umbali mrefu kutafuta chakula, wenzi, na hali nzuri kwa ukuaji wa vipepeo wadogo. Utafiti umeonyesha kwamba, wadudu hawa hustawi vizuri katika hali ya majimaji (chepechepe) na joto la vuguvugu la kati ya 16 hadi 35 °C. Hata hivyo, hali ya baridi na mvua kubwa inawafanya washindwe kuishi.