Tango

Mdudu Kunuka wa Maboga

Coridius janus

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Majani kuwa ya manjano.
  • Maeneo madogo yaliyozama kwenye matunda na mashina.
  • Ukuaji wa mmea unaathirika.

Inaweza pia kupatikana kwenye

5 Mazao
Mung'unye
Tango
Tikiti
Boga
Zaidi

Tango

Dalili

Wadudu wanaonuka, wadogo na wakubwa, wanaweza kusababisha matatizo kwa mazao kwa kunyonya maji ya mimea. Kutegemeana na sehemu wanayokula, husababisha majani kubadilika rangi na kuwa ya manjano na maeneo madogo yaliyozama kwenye mashina na matunda. Ukuaji wa mimea kwa ujumla huathiriwa vibaya. Mazao yanapungua. Wadudu wanaonuka wakiwa wengi, wanaweza kuwa tishio kubwa kwa ukuaji wa mimea midogo na mimea mipya, ukuaji dhaifu.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Mdudu huyu ana maadui wa asili, lakini harufu kali anayoitoa huwa ni kinga kubwa dhidi ya wanyama wanaomla. Pulizia bidhaa zenye mchanganyiko wa mafuta muhimu zenye pyrethrins asilia au mafuta ya mwarobaini. Kumbuka kanuni zilezile za udhibiti wa kemikali. Changanya njia hii ya kupulizia dawa na kuchunguza mazao yako kuona uwepo wa dalili na kuondoa wadudu na mayai yoyote.

Udhibiti wa Kemikali

Daima zingatia mbinu jumuishi zenye hatua za kuzuia pamoja na matibabu rafiki kwa mazingira. Iwapo kuna mashambulizi makubwa, pulizia dawa za kuua wadudu kwa kugusana na wadudu hao ambazo zimeruhusiwa kwa matumizi haya katika eneo lako. Pulizia asubuhi, wakati wadudu waliepevuka wanapokuwa amalia(hai), na elekeza dawa kwenye mizizi na pia upande wa chini wa majani. Iwapo unatumia matandazo ya majani, pulizia maji kwenye matandazo ya majani ili kuwafanya wadudu watoke mafichoni kisha nyunyuzia dawa juu yao.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na mdudu anayeinuka anaefahamika Coridius janus. Mdudu huyu hupatikana zaidi kwenye mimea jamii ya maboga. Wadudu hawa huishi msimu wote wa baridi wakiwa wadudu kamili (waliopevuka) kwenye mabaki ya mimea na kati ya magugu. Kila jike linaweza kutaga hadi mayai 100 chini upande wa chini wa majani, kwenye mashina, au sehemu nyingine za mimea mbadala ambayo wadudu hawa huishi. Mdudu kamili haruki na ana kichwa cheusi, mwili wa rangi ya chungwa, na mbawa nyeusi. Wadudu hawa hupenda kujificha kwenye matandazo ya majani. Wanakuwa kwenye harakati wakati asubuhi na jioni, lakini mchana hujificha upande wa chini wa majani.


Hatua za Kuzuia

  • Epuka kutumia matandazo ya majani karibu na mimea ya jamii ya maboga wakati wa msimu wa ukuaji kwani inatoa nafasi kwa wadudu wa maboga kujificha.
  • Chunguza shamba lako kwani kwa kufanya hivyo kutaepusha uharibifu mkubwa ikiwa utaona na kuondoa wadudu na mayai yao kwa mikono au kwa mitego.
  • Zingatia sehemu za shamba ambazo ziliharibiwa na wadudu wanukao (stink bugs) katika miaka iliyopita.
  • Mara tu unapoona wadudu wakubwa, wachanga, au mayai, waondoe kwa mikono na waangamize.
  • Kila wakati vaa glavu kwani wadudu hawa hutoa harufu mbaya baada ya kuvunjwa.
  • Hakikisha shamba lako ni safi na halina mabaki ya mimea ambayo yanaweza kuwa sehemu za kujificha na kuishi msimo wote wa baridi.
  • Lima shamba lako vizuri baada ya mavuno.

Pakua Plantix