Cricula trifenestrata
Mdudu
Viwavi wanaweza kukata majani yote kutoka kwenye mti na kupunguza idadi ya maua ambayo huzalishwa. Uharibifu unaotokana na ulaji wa viwavi huanza kwenye sehemu za nje za mti na baadaye huenea katikati na juu. Miti iliyoshambuliwa sana huwa dhaifu na inaweza isitoe maua au matunda kabisa.
Ili kudhibiti mashambulizi ya viwavi kwa mikono, tumia tochi yenye mshikio mrefu ili kupasha joto maeneo ambayo viwavi hukusanyika, na kuwafanya waanguke. Kusanya viwavi walioanguka ukiwa umevaa glavu, na uwafukie kwenye udongo. Ondoa na uharibu majani yaliyohifadhi makundi ya viwavi wachanga na mayai. Kwa udhibiti wa kibiolojia, tumia wadudu vimelea kama vile Telenomus sp., wanafaa dhidi ya mayai na pupa, na Beauveria bassiana, ambao hulenga nondo wazima. Wawindaji wa asili pia wana jukumu muhimu katika kudhibiti milipuko. Zaidi ya hayo, dawa za kuulia wadudu zinazotokana na mwarobaini kama vile azadirachtin zimethibitishwa kuwa na ufanisi katika kudhibiti wadudu hawa.
Nondo mara nyingi huweza kudhibitiwa bila kutumia viuatilifu vya kemikali, haswa ikiwa uvamizi utagunduliwa mapema. Kama suluhu ya mwisho, ni vyema kuzingatia mbinu za kikemikali kama vile methyl parathion na endosulfan ambazo zinaripotiwa kuwa na ufanisi mkubwa. Unapotumia dawa za kuua wadudu au bidhaa yoyote ya kemikali, ni muhimu kuvaa mavazi ya kujikinga na kusoma kwa uangalifu maagizo ya lebo. Kanuni hutofautiana kulingana na nchi, kwa hivyo hakikisha unafuata miongozo mahususi ya eneo lako. Hii inahakikisha usalama na huongeza nafasi za matumizi yenye ufanisi.
Minyoo wa chai ni wadudu waharibifu sana kwa miti ya embe hasa Bangladesh, Myanmar, na India, lakini pia wanatoa fursa kwa uzalishaji wa hariri. Viwavi wachanga hula pamoja katika vikundi na kuenea huku wakikua. Wakati hakuna chakula cha kutosha, lava wakubwa wanaweza kushuka kutoka kwenye mti wao na kutambaa kwenye miti mipya ili kutafuta chakula zaidi. Mzunguko wa maisha ya wadudu hawa hujumisha hatua kadhaa. Baada ya kula kikamilifu, kiwavi husokota koko/kiota katika makundi ya majani au kwenye mashina. Nondo waliokomaa ni wa usiku(huwa amilifu wakati wa usiku) na wana rangi tofauti, huku madume wakiwa na madoa mawili meusi kwenye mbawa zao za mbele, wakati majike wakionyesha madoa makubwa yasiyo na mpangilio. Kunaweza kuwa na hadi vizazi vinne kwa mwaka. Licha ya kuwa mharibifu, nondo huyu hutoa hariri ya ubora wa juu. Nchini Indonesia, mdudu huyu amefanywa kuwa muhimu kwa uvunaji wa hariri kwa kiwango kikubwa, na kutoa chanzo cha mapato kwa jamii za vijijini.