Njugu Mawe & Dengu Nyekundu

Mdudu mate

Cercopidae

Mdudu

Kwa Ufupi

  • Dutu nyeupe yenye povu kama mate kwenye shina.

Inaweza pia kupatikana kwenye


Njugu Mawe & Dengu Nyekundu

Dalili

Mwanzoni mwa majira ya kuchipua na majira ya joto/kiangazi, wingi wa dutu nyeupe yenye povu kama mate huonekana kwenye mashina machanga na majani ya mimea. Kila mkusanyiko mweupe una wadudu wadogo wa milimita 4-6 ambao bado hawajakua kikamilifu wenye rangi ya krimu nyeupe. Kawaida ukuaji wa mmea hauathiriwi, lakini, ikiwa wadudu watakuwa wanakula kwenye chipukizi, hii inaweza kusababisha matatizo ya ukuaji.

Mapendekezo

Udhibiti wa Kiasili

Udhibiti wa kibayolojia haupo kwa mdudu huyu mdogo. Ikiwa inahitajika, waondoe kwa mkono.

Udhibiti wa Kemikali

Dawa za kuua wadudu hazihitajiki kudhibiti panzi-vyura na wadudu mate. Dawa za kuulia wadudu hazifanyi kazi dhidi ya wadudu mate kwa sababu wadudu wachanga hulindwa ndani ya dutu yenye povu kama mate hivyo hawawezi kuathiriwa na dawa.

Ni nini kilisababisha?

Uharibifu husababishwa na wadudu mate ambao hunyonya juisi ya mmea. Kawaida hawasababishi uharibifu mkubwa, lakini ikiwa idadi yao itaongezeka, inaweza kuwa shida. Wanaunda dutu yenye povu kama mate ili kujilinda kutoka kwa wadudu/wanyama wanaowawinda. Wadudu mate wana sehemu tatu kwenye mzunguko wa maisha yao: yai, hatua changa, mdudu kamili. Kila hatua inaweza kudumu hadi nusu mwaka. Wakati mayai yanapoanguliwa, wadudu wadogo hula kwenye mmea. Wakati wa awamu yao inayofuata, hutoa povu ili kujilinda na kuendelea kukua hadi wanapokuwa wadudu kamili. Ili kukua, mdudu akiwa katika hatua ya changa huzunguka mmea na kula sehemu tofauti za mmea kwa mwezi 1-3. Wadudu mate wakubwa kawaida hutaga mayai kwenye uchafu wa mimea au kwenye majani na mashina. Kila mdudu mate wa kike hutaga mayai karibu 100-200. Hudumu kama mayai kwa msimu mzima kwenye mimea. Wakiwa kwenye hatua ya uchanga kawaida huwa na rangi ya kijani. Kabla ya kukua na kuwa mdudu kamili, rangi ya mwili inakuwa na weusi na mabawa huanza kukua. Wadudu mate hupendelea kula kwenye mikunde na mimea mingine ya kurekebisha naitrojeni.


Hatua za Kuzuia

  • Ili kuondokana na wadudu mate, unaweza kutumia maji yenye msukumo mkali ili kuosha povu na kudondosha wadudu mate kutoka kwenye mmea.
  • Safisha shamba lako baada ya msimu wa mazao kuisha ili kupunguza uwezekano wa mayai kuendelea kuwepo hadi msimu ujao.
  • Wakati wa majira ya kuchipua, angalia wadudu mate kwenye magugu na uwaondoe kabla ya wadudu hao kuenea kwenye mazao yako.

Pakua Plantix